Akizungumzia uamuzi wake wa kuhamia 
ndondi za kulipwa, Mnyeto anasema kuwa alifanya hivyo kama sehemu ya 
hatua za maisha yake katika mchezo huo aliodai kuwa anaupenda mno. 
“Nimekuwa katika ngumi za ridhaa kwa muda mrefu, na sasa nimeamua 
kuhamia ndondi za kulipwa, nikiamini ninaweza kupata mafanikio makubwa 
kwani nina usongo wa kulipa sifa Jeshi la Polisi pamoja na nchi yangu 
kwa kufanya mambo makubwa kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa. 
“Katika maisha yangu ya ndondi, nimekuwa nikipata sapoti ya hali ya juu 
kutoka kwa mwajiri wangu na wachezaji wenzangu ambao nao ni askari 
Polisi… naondoka ngumi za ridhaa kwenda za kulipwa, nataka kurejesha 
hadhi ya ndondi ndani ya Jeshi la Polisi. “Matarajio yangu ni kufuata 
nyayo za Haji Matumla ambaye ni askari Polisi, Yombayomba (Michael) na 
wenginbeo, ikiwezekana hata kuwazidi, naamini hilo linawezekana kama 
kila kitu kitakwenda kama nilivyopanga.” Aliongeza: “Nataka kufanya kitu
 tofauti, nashukuru hata rafiki na ndugu zangu, wananisapoti, sitaki 
kubahatisha, ndio maana nimetafuta kocha mzuri mwenye uzoefu, kama 
Rashind Matumla, ambaye nashukuru amenipokea na kunikaribisha katika 
‘gym’ yake. “Kwangu Rashid Matumla ni mtu muhimu sana, nimekuwa 
nikimshabikia tangu nilipokuwa mtoto na nilitamani siku moja nije kuwa 
kama yeye au hata kumzidi. “Kufanya mazoezi katika ‘gym’ yake (Matumla),
 kunanisisimua sana, ninapoona picha zilizopo katika ukuta wa gym yake 
akiwa anapigana, akiwa amebeba mikanda mbalimbali ya ubingwa wa Dunia, 
na hata habari za kwenye magazeti za kumpongeza, ninapata hisia kali 
sana.” Anasema kuwa kikubwa zaidi, ni kuona bingwa huyo wa zamani wa 
Dunia wa WBU ambaye alishiriki mara tatu michezo ya Olimpiki, mwaka 
1988, 1992 na 1996, akimpa moyo wa kufuata nyayo zake “Kaka Rashid 
amekuwa akinipa moyo kuwa kutokana na jinsi alivyoniona, ninaweza kuwa 
bondia mzuri kama yeye au hata kumzidi, lakini kama nitafanya bidii 
katika mazoezi, kuzingatia nidhamu na miiko ya mchezo huu wa ngumi.” 
Mnyeto anaelezea hali ya ndondi ilivyo ndani ya Jeshi la Polisi, 
akisema: “Polisi kuna wachezaji wazuri sana, tatizo ni hamasa, hivyo 
nimeona ni vyema nikawafungulia njia wenzangu kwani hakuna sababu yoyote
 ya kutofika mbali katika mchezo huo, maana mwajiri wetu anajali sana 
michezo si kama katika sekta nyingine.” Kwa upande wa ndondi za ridhaa, 
anasema kuwa tatizo lililoko huko ni uongozi wa chama husika kutokuwa na
 mikakati ya kuuendeleza mchezo huo. “Katika ngumi za ridhaa hapa 
nchini, tatizo ni uongozi, pale kuna mtu mmoja tu, Mashaga (Makore), 
jamaa anajitahidi sana kupambana, kama angepata msaada, basi mambo 
yangekuwa mazuri zaidi,” anasema. Na sasa Mnyeto ni ‘hakuna kulala’, 
kila baada ya kumaliza majukumu yake ya kikazi, hugeukia mazoezi ya 
ndondi katika gym ya Matumla na wakati mwingine kwenda kwenye klabu 
nyingine za mazoezi. Katika mazoezi yake hayo, wakati fulani amekuwa pia
 akinolewa na Haruna Andrew ‘Ndimu Mkata Shombo’ ambaye naye ni bondia. 
Matarajio yake kwa siku chache zijazo ni kupata pambano la kujipima 
nguvu dhidi ya bondia atakayejitokeza kukabiliana naye. “Kabla ya kupata
 pambano, niliona ni vyema nikajifua kwanza kwani kuna kipindi 
nilisimama kufanya mazoezi, hivyo lazima niwe fiti kabla ya kupanda 
ulingoni,” anasema. Anasema kuwa matarajio yake mapema mwezi ujao 
atakuwa fiti tayari kuonyesha ubabe na bondia yeyote atakayekubali 
kupigana naye. Hata hivyo, alisema kuwa katika kufanikisha azma yake 
hiyo, hatasita kuwa bega kwa bega na mwajiri wake ambaye ni Jeshi la 
Polisi kuhakikisha kipaji chake hicho hakiathiri majukumu yake ambayo 
ndiyo yanayomwezesha kufanikisha baadai ya mambo kuelekea mkakati wake 
wa kuwa bondia hatari hapa nchini. “Pamoja na haya yote, ninaiheshimu 
sana kazi yangu kwani ndiyo inayonifanya niwe na jeuri ya kutamba kutaka
 kufuata nyayo za akina Matumla, bila Jeshi la Polisi, nisingekuwa kama 
nilivyo sasa,” anasema Mnyeto. Bondia Yusuph Mnyeto, alizaliwa Februari 
20, mwaka 1982 katika eneo la Ngamiani, jijini Tanga, akiwa ni mtoto w 
asaba katika familia ya watoto saba wa Mzee Mnyeto. Alianza masomo yake 
katika Shule ya Msambweni, jijini humo na baadaye kujiunga na Chuo cha 
Ufundi Stadi (VETA) mwaka 1995.Mnyeto ambaye kwa sasa hajaona, lakini 
akiwa na mchumba anayetarajia kufunga naye ndoa muda si mrefu, alijiunga
 na Jeshi la Polisi mwaka 2000 na hadi sasa analitumikia jeshi hilo, kwa
 umakini na uadilifu wa hali ya juu. Pamoja na kulitumikia Jeshi la 
Polisi na kuendeleza kipoaji chake cha ndondi, Mnyeto anekuwa akitenga 
muda wake kwa ajilki ya kujiendeleza kimasomo. “Kama unavyofahamu, elimu
 ni kila kitu na haina mwisho, nashukuru mwajiri wangu (Jeshi la 
Polisi), hana kikwazo na mtu anayetaka kujiendeleza kimasomo, kwa kweli 
ninashukuru sana kwa hilo,” anasema Mnyeto. Juu ya mkakati wake wa 
kuendelea na masomo, anasema: “Ndondi inaonekana kama ni mchezo wa akina
 ‘Kayumba’ (watu wasio wasomi), tusikubali ujinga, mabondia twendeni 
shule.” Kuhusiana na malengo yake baada ya kuanza kupata mafanikio 
katika ndondi, anasema amepania kufungua klabu yake ya mazoezi ya ndondi
 (gym) ambayo itakuwa katika ubora wa hali ya juu ili kuwawezesha vijana
 chipukizi kujinoa waweze kutimiza ndoto zao. “Lengo langu ni kufungua 
‘gym’ ambayo itakuwa na hadhi ya kimataifa, kama ilivyo Azam Complex ya 
klabu ya soka ya Azam. Juu ya kilio cha mabondia wengi kutaka wadhamini 
kujitokeza katika mchezo huo, Mnyeto anaasa: “Tusitegemee zaidi 
wadhamini, tujitegemee, tusipigane kuganga njaa, kwani tunadhalilishwa 
kwa kutojitambua, maana ukipigwa unajirudisha nyuma na umaarufu wako 
unapotea.”  tunamtakia kila la kheri Yusuph Mnyeto kuelekea 
jitihada zake za kuwa bondia wa kulipwa mwenye mafanikio hapa nchini, 
tukiamini hilo linawezekana iwapo atajipanga hasa na kuzingatia miiko ya
 mchezo huo.BONDIA YUSUPH MNYETO ANGIA NGUMI ZA KULIPWA RASMI
 - 
                          
14:53

 mchezo huo.
0 comments:
Chapisha Maoni