ASKARI WA JESHI LA POLISI TANZANIA AFIKISHWA MAHAKAMANI,KESI YAKE YA KWANZA AHUKUMIWA MIAKA 30

Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Mbeya Mjini Pc Jamse pamoja na wenzake wanne ambao ni raia wa kawaida wanakabiliwa na Shitaka la kuteka Loli lenye namba za usajiri T790CMW/T620CJW Mali ya Kampuni ya usafirishaji ya A A Transporter ya Mkoani Mbeya mjini.

Ilikuwa siku ya Tarehe 7/10/2013 ambapo Dereva wa loli hili nd.JosephTomath alienda katika kampuni ya kuhifadhi Kahawa ya City Coffee Iyunga iliyopo Mbeya Mjini kupakia kahawa kwa ajiri ya kuisafirisha toka Mbeya kwenda Dar es Salaam katika kampuni ya Mawenzi Coffee Exporters ya Mjini Dar es Salaam.
Ilipofika mida ya saa 4.30 jioni alimaliza kupakia Magunia 499 ya Kahawa yenye thamani ya sh.119m na kila Gunia likiwa na kilo 60 ambapo Dereva Joseph Tomath alianza safari ya kuelekea kwenye yadi ya Kampuni sehemu ya Soweto Mbeya Mjini ndipo alipotoka getini katika rami Gafra ilikuja Gari ndogo aina ya saloon kwa mbele na kumzuia asiondoke na wakashuka watu wawili ambapo kwa maelezo ya Dereva huyu alimtambua Pc Jamse ambao walimfuata Dereva na kumuuliza kwanini ameziba njia ndipo Pc Jamse alimwamulu Dereva Timoth ashuke katika loli lake na kumfunga Pingu na Kumuingiza katika gari lao.

Gafra alipoingizwa katika gari hiyo ndipo alifungwa Vitambaa na Bandeji Machoni na Kichwani kisha kupelekwa Sehemu isiyojulikana,Walipofika huko dereva aliteswa na kupelekwa katika msitu wa Senjere Wilayani Mbozi na kutelekezwa huko katika Msitu huo.

Kwa maelezo ya Muwakirishi wa Kampuni hii ya Usafirishaji yenye namba za usajiri no.111685150 nd.Muntazir Kassama alisema kuwa ilipofika mida ya saa 11 jioni ndipo aliamua kumpigia Dereva wake ili ajue amefikia wapi toka atoke pale sehemu ambayo kapakia ndipo alipompigia simu dereva kwa bila ya mafanikio simu iliita bila ya kupokelewa.Ilipofika mida ya saa 12.30 jioni alipiga simu ya dereva ikawa haipatikani ndipo ulivyofika mda wa saa 1.54 alipata ujumbe katika simu yake ya kumjurisha kuwa simu ya dereva Tomath haina chaji.

Ilipofika mida ya saa 2 ndipo nd. Muntazir alipoamua kumtumia ujumbe ambao ulikuwa hewani ili akipatikanika aweze kumpigia ili ajue huyu dereva yupo wapi na alivyoutuma akaamua kujipumzisha ili kukicha ajue aanzie wapi kumtafuta dereva kama alikuwa amepata matatizo.

Ilivyofika mida ya saa 12.45 alfajiri nd.Muntazir Kassama alipokea simu ya mtu ambaye alijitambulisha kama anaitwa Joseph Tomath ambaye alisema kuwa ametekwa na watu wasiojulikana mitaa ya iyunga na kumpeleka sehemu isiyojulikana huko katika misitu ya mlima senjere Wilayani mbozi.Baada ya hapo dereva aliamua kwenda kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha songwe na kumuelezea kitu kilichomtokea na ndipo mwenyekiti huyu alipoamua kwenda katika barabara ya senjere ndipo walipolikuta loli limetelekezwa pale likiwa halina mzigo wowote ule wa Kahawa.

Baada ya hapo Mwenyekiti aliamua kumpigia simu bwana Muntaziri ambapo namba zake alizipata ubavuni mwa loli lile ambapo alimtaarifu kuwa loli lake limetelekezwa sehemu hiyo na likiwa halina kitu chochote mpaka nyaraka walizichukua ili kupoteza ushahidi.

Baada ya hapo nd.Muntazir aliamua kwenda polisi na kuwaeleza mkasa mzima ndipo askari wakaamua kwenda mpaka sehemu ambayo loli lilipatikana na kuamua kumshikiria dereva wa loli hilo kwa uchunguzi zaidi.Mara baada ya dereva kushikiriwa na Jeshi la Polisi katika kituo kidogo cha songwe ndipo askari wa Jesh hili waliaamua wampeleke katika kituo kikubwa cha Polisi kilichopo Mbeya Mjini kwa Maojiano zaidi.
Walipofika pale dereva alihojiwa  na maelezo yake kuchukuliwa jinsi ilivyokuwa na kupekekwa Mahabusu katika Gereza la Luanda lililopo Mbeya Mjini.Baada ya hapo ilipofika tarehe  3/01/2014 Pc Jamse akishirikiana na wenzake wawili mmoja akiwa askari Magereza walienda kufanya tukio la ujambazi katika Barabara inayotoka Mbeya mjini kwenda Chunya kupitia Isanga.

Walienda kuwapola pesa Wafanyabiashara wa Madini wa jamii ya kihindi waliokuwa wakienda Chunya kununua Madini ania ya dhahabu.Wafanyabiashara hawa gafra walipokuwa katika safari yao katika maeneo ya isanga kwa mbele walivamiwa na majambazi hawa na kuwaamuru washuke kwenye gari na kuwapora vitu vya thamani kama raptop,simu za mkononi,na kwa bahati nzuri fedha hawakuweza kuwapora kutokana waliziweka benki ndipo mmoja wao alifanikiwa kukimbia na kuamua kupiga simu polisi ndipo polisi wa mbeya mjini wakaamua kuwapigia simu polisi wa chunya ili waweze kuja ili wawakamate katikati.


 Baada ya askari polisi toka kila pande mbili kuwakuta wakina pc Jamse wakiwa na bunduku ndipo wakafanikiwa kumpiga risasi ya kwenye paja jambazi mmoja ndipo wakatiwa chini ya ulinzi na kufikishwa Polisi mbeya mjini na kisha kupelekwa Mahakama kuu ili kujibu mashtaka yaliyowafanya kuhukumiwa miaka 30 kila mmoja aliyehusika kutokana na ushahidi uliopatikana toka kwa maaskari waliowakamata na baadhi ya vitu vya wafanyabiashara hawa vilivyokutwa katika gari ndogo ambayo waliitumia kwa uharifu huo siku hiyo.

Baada ya kupelekwa katika gereza la luanda ndipo yule dereva alipomtambua Pc Jamse na kuwaita askari magereza na kuwaeleza kuwa Mmoja wa watu waliomkaba ni huyu hapa pc Jamse na walipoamua kuripoti kwa wapelelezi wa kesi hii iliyokuwa ikimuhusu huyu dereva  Joseph Tomath dhidi ya kampuni ya AA Transporter kuhusu kuibiwa kwa kahawa mali ya Mawenzi Coffee Exporters.

Baada ya hapo ndipo askari wakaamua kumjurisha mwakirishi wa kampuni hii ya AA Transporters nd.Muntazir Kassama kuwa wale Majambazi waliopola mzigo wake wa kahawa pale senjere wamepatikana na wapo gerezani luanda kwa kesi nyingine ambayo wamehukumiwa miaka 30 kila mmoja mmoja wao ni askari wa jeshi la polisi Pc Jamse na mwingine ni askari Magereza.

Baada ya watuhumiwa kurudishwa polisi kwa Maelezo zaidi ndipo dereva alivyoitwa na kutoa maelezo ambayo alisema kuwa alimtambua Pc Jamse na dada mmoja ambaye anarasta ambaye baada ya uchunguzi kufanyika alikamtwa na kuwekwa katika gwaride la utambulisho ambapo waliwekwa madada wengi wenyerasta ndipo dereva akamchagua dada ambaye mara nyingi huwa alikuwa akionekana na Pc Jamse katika sehemu mbalimbali na gari ndogo hiyo hiyo ambayo waliitumia kuwavamia wafanyabiashara wa madini na ambayo waliitumia kumteka dereva wa loli na kupora magunia ya kahawa.

Baada ya kukamtwa kwa dada huyu kwa jina akijurikana kama Gwantwa mkazi wa Jakaranda ndipo jeshi la polisi likaamuwa kuwafikisha mahamani kujibu mashtaka yanayowakabili ambapo mpaka hivi sasa huyu dada yupo mahabusu katika gereza la luanda na wakina pc Jamse wakiwemo humo humo wakiwa wafungwa kwa kesi ya kwanza na mahabusu kwa kesi ya pili ambayo mlalamikaji ni kampuni ya usafirishaji ya AA Transporters ya Mjini Mbeya.Mpaka sasa watuhumiwa wapo watano kwa kesi hii ya pili na kesi imeahirishwa mpaka tarehe 30 mwezi huu wa 4 katika mahakama kuu mkoani mbeya.

                            Imetayarishwa na Briany Willfredy toka Mbeya..........................................
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List