Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba akizungumza katika mkutano wa
waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es
Salaam katika kutoa tamko rasmi za tathimini ya Jukwaa la Katiba
Tanzania kuhusu Katiba Mpya, Tulipotoka, Tulipo na Tuendako. Pembeni ni
Msimamizi wa Mradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya (NGO Network for
Dodoma) Bw. Edward Mbogo (kushoto) na Mjumbe wa Jukwaa la Katiba toka
Pemba Bw. Omari Omari.
Waandishi wa Habari wakifuatilia.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Jukwaa
la Katiba Tanzania (JUKATA) limejitolea kuratibu maridhiano miongoni
mwa makundi ya kisiasa asasi za kiraia, asasi za wananchi na taasisi
zote za muhimu zilizoguswa na migogoro inayoendelea katika Bunge maalum
la katiba Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es
Salam, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Deus Kibamba juu ya tathimini
walizozifanya katika bunge hilo wameamua kujitolea kufanya maridhiano
hayo kwa kuwashirikisha viongozi maarufu Afrika Mashariki akiwemo
mheshimiwa jaji mkuu mstaafu wa Tanzania, Barnabas Samatta ambaye
atakuwa mkuu.
wa jopo hilo la usuluhisho na ndugu Patrice Lumumba kutoka nchini Kenya ambaye atakuwa msaidizi.
Aidha
jukwaa hilo limeonyesha masikitiko yake kwa kile alichookiita ni
uvunjifu wa kanuni mara baada ya wabunge zaidi ya mia mbili kutoka nje
lakini wabunge waliobakia kuendelea kurekebisha kanuni za bunge hilo
jambo ambalo wamesema kuwa haikustaili kwani wana uwezo wa kujitungia
sheria.
Kibamba
amesema kuwa kutokana na mwenendo wa bunge hilo hadi hapa lilipofikia
wabunge hao hawana nia ya dhati ya kulipatia taifa katiba mpya huku
akitolea mfano kuwa katiba mpya ilipangwa kuwekwa saini na Rais siku ya
tarehe 26 mwezi huu yani leo lakini hadi sasa hata majadiliano ya sura
mbili hayajamalizika, na kuwahakikishia watanzania kuwa hakuna katiba
mpya itakayopatikana kwa mwaka huu.
Hata
hivyo mwenyekiti huyo amewataka wajumbe wote na asasi zote zilizopo nje
ya muendelezo wa bunge hilo maalumu la katiba kuwa tayari kwa maridhiano
kwa mtu au taasisi yoyote atakayekuwa tayari kutatua migogoro yao ili
kuwezesha upatikanaji wa katiba kwa taifa letu.
0 comments:
Chapisha Maoni