KAMA MWANAE AKIPATA HESHIMA HII,ATAHAKIKISHA HAPATI AIBU KWA WANANCHI.

Naibu Katibu Mkuu Bara wa Jumuiya ya Wazazi Taifa mh.Glorious Bernard Luoga akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (W) ya Bagamoyo Abdurashid Shariff Zahoro wakiangalia jengo la Jumuiya ya Wazazi lililopo Kata ya Miono Jimbo la Chalinze lililojengwa kwa nguvu ya Wazazi  wa Jumuiya hiyo


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Abdurashid Shariff Zahoro mbele akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa pwani Mh.Jackson J.Kituka Katikati na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Bara Taifa Mh.Glorious B.Luoga wakiwa kwa pamoja katika kuhakikisha Wazazi wa Kata ya Miono wanamchagua Ridhiwan M.Kikwete anakuwa Mbunge wa wa Jimbo la Chalinze.

Hili ndio Jengo la Jumuiya ya Wazazi likiwa katika kata ya Miono ambalo halijamalizika ambapo Mama Salma Kikwete aliahidi atachangia Sh.3m ili Jumuiya hiyo iweze pata Ofisi Katika kata ya Chalinze.
Wana Jumuiya ya wazazi wakiwa kwa Pamoja katika kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwan M.Kikwete katika kata ya Miono.
Wazazi wa kata ya Miono wakiwa katika Kikao Cha Jumuiya ya Wazazi  walipotembelewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Bara Taifa Katika kampeni za Kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Abdurashidi Shariff Zahoro akihojiwa na Waandishi wa Habari Gloria matola wa Star Tv na Omary Mngindo wa gazeti la majira kuhusiana na ni vipi wataweza kuzitatua Changamoto za Wazazi hao pindi Ridhiwani Kikwete atakapo kuwa Mbunge wao
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi  CCM Bara Taifa akiongea na Wazazi wa Kata ya Miono kuhusiana na kumchagua Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete ili awe Mbunge wao siku ya Uchaguzi utakaofanyika Tarehe 6 Jumapili.Aliwaomba wajitokeze kumpiga Kura kwa wingi.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Bara nd.Glorious B.Luoga akiwa Sambamba na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Bagamoyo Mh.Abdurashid Shariff Zahoro wakiwatunza waimbaji wa Kikundi cha Ngoma za Asili Katika kata ya Mkange Walipotembelewa na Jumuiya ya Wazazi.
Katibu wa CCM Wilaya ya Same Kilimanjaro akifafanua jinsi ya Kumchagua nd.Ridhiwani Kikwete katika Karatasi ya kupigia Kura kwa wananchi wa kata ya Miono katika Jimbo la Chalinze.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Bagamoyo Mh.Abdurashid Shariff Zahoro akimweleza mambo mbalimbali Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya CCM Bara kuhusu Wananchi wa Kata ya Mkange kwa Jinsi gani watakavyo mchagua Ridhiwani Kikwete awe Mbunge wao Siku ya Tar.6 Jumapili
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi CCM Bara nd.Glorious B.Luoga akiulizwa Maswali na Waandishi wa Habari jinsi gani Ridhiwani Kikwete atakavyotatua Kero za Wananchi wa Kata za Mkange na Miono siku akichaguliwa kuwa Mbunge wao.
Katibu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Nd.Swalla akiwa na Madereva wa CCM kwa Furaha wakicheza Mziki kumfurahia Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze CCM Ridhiwani M.Kikwete ili awe Mbunge wa Jimbo ilo katika kata ya Mkange
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Bagamoyo mh.Abdurashid Shariff Zahoro akiwaongoza Wananchi wa Kata ya Mkange Sara ya Kumuombea Mgombea wao Ridhiwani Kikwete ili awe Mbunge wao katika Uchaguzi utakaofanyika siku ya tar.6 Jumapili.

Nabu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Bara akiwahutubia Wananchi wa Kata ya Mkange kuwaomba siku ya Uchaguzi waweze kujitokeza kupiga Kura Ili wamchague Ridhiwani Kikwete ili awe Mbunge wao wa Jimbo la Chalinze.

Katika kuhakikisha wazazi wa kata Mkange na Miono wanamchagua Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani M.Kikwete anakuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mwenyekiti wa Wilaya ya Bagamoyo mh.Adburashuid Shariff Zahoro akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Bara nd.Glorious B.luoga waliwatembelea Wananchi wa Kata za Miono na Mkange ili kuwahimiza kuwa sku ya tar.6 wajitokeze kwa wingi wamchague Ridhiwani Kikwete awe Mbunge wao.

Wakijibu kwa Ufasaha zaidi Changamoto ambazo zinawakabili Wananchi wa Kata hizo ambazo Kama Ridhiwani M.Kikwete wakimchagua ili awe Mbunge wao ataweza kuzitatua na Wananchi hao kupata Maendeleo Kwa Kasi zaidi.

Changamoto kubwa ambayo inawakabiri wananchi wa Kata hizo ni kuhusiana na Shule ya Sekondari Kaole ambayo zamani ilikuwa Chini ya Jumuiya Ya Wazazi ambapo hivi sasa inamilikiwa na Mtu binafsi ni vip Shule Hiyo itaweza kurudi Mikononi mwa Wazazi?

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Bagamoyo alisema kuwa Pindi Wananchi wakimchagua Ridhiwani Kikwete awe Mbunge wao atahakikisha anashirikiana nae kuirudisha Shule hiyo Mikononi mwa Wazazi kwani Swala hilo Ridhiwani analifahamu na kabla ya hapo alikuwa analishughurikia kisheria.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM bara aliwaambia Wananchi wa Kata hizo kuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Ridhiwani Mrisho Kikwete ndiye Dawa ya Matatizo yao kwani ni Msomi Mwanasheria ambaye wanatakiwa wamchague kwa kumpigia kura ili aweze kutatua Changamoto zao kama  Zifuatazo:

MAJI))))))) Akizungumza kwa furaha Naibu Katibu Mkuu alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa ni mzariwa wa Tanzania ni mzaliwa wa Jimboni hapa na "Kama mwanae akipata Heshima hii,atahakikisha hapati aibu"kwa maana ya kuwa ataweza kulete maji katika Kata hizo na jimboni kote ii atimize yale yote mwanae aliyoyaahidi kwa Wananchi wa Jimbo la Chalinze.

ELIMU))))) Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Bara pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Bagamoyo Abdurashid Shariff Zahoro waliwaambia wananchi kuwa ni Vema wakaa na Vijana wao na Kuwashuri siku ya Tarehe 6 waweze kujitokeza Kumchagua Ridhiwan Kikwete awe Mbunge wao ili aondoe tatizo la elimu kuwa chini kwa kujenga Madarasa,Mabweni,Shule na kuweka waalimu wa kutosha ili watoto wapate elimu bora.

ZAHANATI))))))))Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi waliwaambia kuwa wanatakiwa wamchague Ridhiwani ili awe Mbunge wao aondoe tatizo la Wanawake kufariki Njiani pindi wanavyoenda kwa umbali mlefu kujifungua au kujifungulia njiani.Ridhiwani Kikwete atajenga Zahanati na kuweka Wauguzi na Ndiomaana ameweza kusaidia Jengo la Jumuiya ya Wazazi kata ya Miono kujengwa na Mama yake Mama Salma Kikwete kuaidi sh.milion 3 ili Jengo ilo liwee kukamilika haraka ipasavyo.

                             Imeandikwa na Briany Willfred
                                         Nani kama MAMAAAAAAAAAAAAAAA????
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List