Hussein Jumbe 'Mtumishi' |
Ishi Mashauzi atakayemsindikiza Hussein Jumbe na Talent Band |
Akizungumza na MICHARAZO, Mkurugenzi wa Talent Band, Hussein Jumbe alisema kuwa uzinduzi huo utafanyika Aprili 30 kwenye ukumbi maarufu Kisuma Night Park lililopo eneo la Temeke Mwembeyanga na watasindikizwa na makundi hayo mawili.
Jumbe alisema pia bendi yake ya zamani ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' watakuwepo ukumbini kumpiga tafu kwenye uzinduzi huo wa aina yake.
"Natarajia kufanya uzinduzi wa albamu ya bendi yetu ya Talent iitwayo 'Kiapo Mara Tatu' na makundi ya Mlimani Park, Mashauzi Classic na Ngoma Afrika watanisindikiza siku hiyo pale Mwembeyanga," alisema.
Jumbe alisema kuwa, maandalizi ya uzinduzi huo unaendelea vyema na kuwataka mashabiki wa muziki wa dansi kujitokeza kupata burudani ambayo wameikosa kwa muda mrefu jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni