Amir Khan |
LAS VEGAS,
Marekani
LEO katika
maisha ya wenzetu tutakuwa na bondia wa Uingereza Amir Khan ambaye hivi
karibuni amefanikiwa kumchapa Luis Collazo.
Mbabe huyo
amefanikiwa kuonesha kwamba bado makali yake yana uhai katika pambano hilo
baada ya kufanikiwa kumlambisha vumbi mpinzani wake huyo katika pambano
lisilokuwa la ubingwa.
Khan
amejikuta akicheza pambano hilo kwa ustadi kutokana na kutafuta nafasi ya
kucheza na Mayweather ambayo miezi 12 nyuma ilionekana kuyeyuka baada ya
kutocheza na bondia yeyote.
Kwa kuonesha
kwamba amedhamiria kucheza na Mayweather Jr, baada ya kushinda pambano hilo
alisikika akisema kuwa bondia anayemtaka kwa sasa ni mbabe huyo asiyepigika.
Alisema “kwa
sasa naamini watu watakuwa wakitaka kushuhudia pambano langu na Floyd ambaye
naamini nitamchapa kirahisi kutokana na umri wake kuwa mkubwa,”.
USICHOKIJUA
Ingawa watu
wengi hufikiria kwamba Khan ni raia wa nchi za Asia lakini kijana huyo
amezaliwa na kukulia Bolton, England, na wazazi wenye asili ya kipakistan
wanaotokea katika jamii ya Punjab.
Khan ni
muumini wa dini ya kiislam, na amekuwa akisaidia katika kuiwezesha tuzo
inayotolewa na waislama wa nchini humo inayokwenda kwa jina la ‘Muslim Writers
Awards’.
han anatoka
katika familia yenye watoto wanne ambako ana dada wawili na kaka mmoja, Haroon ‘Harry’
Khan, mbabe asiyepigika.
Amir Khan ni
mdogo wa mbabe na mshindi wa medali ya Olympic ya Uingereza, mshindi wa medali
ya fedha ya olimpiki ya mwaka 2004 wakati akiwa na miaka 17.
Khan ana
historia ya kukamata ubingwa wa dunia wa WBA akiwa na umri mdogo kuliko
mwingireza mwingine wakati huo aliuchukua akiwa na miaka 22.
Ukiachilia
ngumi ni mpenzi wa mchezo wa Kriketi, mpira wa kikapu na soka akiwa shabiki wa
klabu ya Bolton Wanderers.
Mwaka 2012, alikuwa
katika picha ya pamoja katika akaunti yake ya Twitter ikimuonesha akiwa na wachezaji
wa Manchester United, Rio Ferdinand, Alex Buttner, Michael Carrick na David De
Gea.
Lakini
pamoja na kuonekana akiwa na nyopta hao huku akiwa amevaa jezi ya klabu hiyo
lakini Khan alisema kuwa 'pamoja na kufanya hivyo lakini mimi bado ni shabiki
wa klabu ya Bolton kwa njia yoyote.'
MSAADA WA KIJAMII
Khan amekuwa
mtoaji mzuri wa misaada kwa watu wenye mahitaji kwa mfano mwaka 2004 alitoa
msaada wa Euro milioni 1 kwa familia za wahindi waliokumbwa na tetemeko la
Tsunami nchini India.
Katika mwaka
huo alikwenda nchini Pakistan na kutoa vyakula katika kambi za watu waliokuwa
wameathiriwa na tetemeko la Kashmir.[
Desemba
2013, Khan aliongoza harambee ya kuchangia Umoja wa waislam kutoka Ufilipino
kwa ajili ya kutoa msaada wa waathirika wa tetemeko la Typhoon Haiyan na
walikusanya kiasi cha Euro 83,400.
JINAI
Oktoba 23,
2007 Khan alitiwa mbaroni kwa kuendesha kwa kasi na alifikishwa katika mahakama
ya Bolton kujibu shtaka lake ambako alifungiwa kuendesha gari kwa muda wa miezi
sita ikiwamo na kupigwa faini ya euro 1000.
Mwaka 2006
aliwahi kupigwa faini ya Euro 40,000 kwa kosa la kuendesha kwa kasi.
Januari 7,
2008 Khan alipigwa faini ya Euro 1000 na kufungiwa kuendesha gari kwa siku 42.
Kama
ilivyokawaida mwenye tabia yake hawezi kuacha Julai 12, 2009 Khan alijikuta
akipata ajali ingawa hakufikishwa katika vyombo vya sheria.
MAHUSIANO
Januari 29,
2012 Khan alifunga ndoa na mwanamke wa Marekani mwenye asili ya Pakistani,
Faryal Makhdoom katika harusi ya kifahari iliyohudhuriwa na ndugu na marafiki
waliofikia 1000 akiwamo bondia Ricky Hatton.
Wawili hawa
walifanya sherehe ya harusi yao Mei 31, 2013 huko Waldorf Astoria jijini New
York, Marekani.
Baada ya
kumalizika kwa sherehe hiyo ya kifahari wawili hawa walichukua ndege na kwenda
nyumbani kwao na Khan huko Bolton kwa ajili ya kufanya sherehe nyingine ya
kimila iliyofanyika Manchester na kuhudhuriwa na wageni 4,000.
FEDHA
Mbabe Amir
Khan anamiliki utajiri unaofikia dola
milioni 23 (sawa na shilingi bil 36.8).
MAKAZI
Mbabe Amir
Khan ana mjengo wa maana ambao hajaweka thamani yake lakini pia anamiliki gari
mbalimbali ikiwamo Range Rovers, Bentley Continental, New Mercedes CLS63, Audi
R8, Lamborghini Murcielago na Can-Am Spyder.
WASIFU
JINA: Amir
Iqbal Khan ‘King’
KIMO: Futi 5 na inchi 9
UMRI: 27
Mapambano ya kucheza: 31
Ushindi: 28
KO: 20
Poteza: 3
Sare: 0
Makala hii imeandaliwa
na Shabani Matutu.
Amir Iqbal Khan ‘King’ |
0 comments:
Chapisha Maoni