Tingatinga
la Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] likibomoa moja ya nyumba
zilizopo katika hifadhi ya Barabara inayotarajiwa kuanza kujengwa havi
karibuni, ambapo zaidi ya nyumba 65 zilibomolewa katika eneo hilo la
mlamwa kusini.
Wanawake
wa mtaa wa Mlimwa wakimsaidia Mwenzao aiyezilai baada ya Tingatinga la
CDA kufika kwa ajili ya kubomoa nyumba yake kwa ajili ya kupisha ujenzi
wa Barabara, zoezi hilo lilifanyika Jana ambapo nyumba zaidi ya 65
zilibomolewa na kuacha familia zaidi ya 150 zikikosa makazi.
Mwenyekiti wa mtaa huo Zubeda Haji akielekeza jambo wakati wa ubomoaji huo.
Wananchi
wa Mlimwa waking'oa mabati muda mfupi kabla ya Tinga tinga la CDA
kufika na kuibomoa nyumba hiyo ili kupisha hifadhi ya Barabara
Bibi huyu mkazi wa Mlimwa Kusini ambaye hakufahamika jina lake akiwa
hajui la kufanya baada ya nyumba yake aliyokuwa akiishi iliyojengwa kwa
mtindo wa Tembe huku akiachwa na vyombo vyake alivyoweka kwenye shamba
la mahindi baada ya CDA kufanya uvunjaji huo kwa nyumba zote zilizopo
katika hifadhi ya Barabara.
0 comments:
Chapisha Maoni