Jokate
Mwegelo akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika
kongamano la 2014 Market Forum lililofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah.
Mrembo na mbunifu wa mitindo huyo aliwataka wanafunzi wajiajiri mara
wamalizapo masomo yao kutokana na ugumu wa soko la ajira.
Jokate
Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam iliyoandaa kongamano la 2014 Market Forum
lililofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah. Mrembo na mbunifu wa mitindo
huyo aliwataka wanafunzi wajiajiri mara wamalizapo masomo yao kutokana
na ugumu wa soko la ajira.
Jokate
Mwegelo akiwa na mshindi wa shindano la ubunifu, Jacqueline Rimoi
ambaye alimzawadia sh, 300,000 kwa kutengeneza tangazo la kunadi bidhaa
za kidoti kwenye ukumbi wa Nkrumah.
**********************************************
Na Mwandishi wetu
Mbunifu
wa mitindo na Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 ametoa wito kwa
wanafunzi wanao hitimu vyuo vikuu nchini kujihusisha na ujasiliamali na
kutumia vilivyo vipaji vyao katika kupambana na soko la ajira.
Joketi
alitoa wito huo juzi wakati akitoa mada ya jins ya kujiajiri mara baada
ya kumaliza masomo ya elimu ya juu katika kongamano la wanafunzi wa
chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) lijulikanao kwa jina la 2014 Market
Forum.
Alisema
kuwa pamoja na yeye kusomea mambo ya siasa na kuhitimu digrii yake
chuoni hapo, mpaka sasa hajaweza kufanyia jambo lolote taaluma hiyo
zaidi ya kujiajiri kupitia kampuni yake ya Kidoti Tanzania Limited
ambayo inamuingizia fedha.
Alifafanua
kuwa hatua hiyo imekuja kutokana na ugumu wa soko la ajira na kutokana
na kuamua kujiajiri kwa njia mbadala (vipaji) vyake.
“Wakati
nasoma, lengo langu kubwa lilikuwa ni kuwa mwanasiasa, nilimaliza hapa
hapa Chuo Kikuu na baadaye nilishauliwa nichukua ‘masters’, nilianza
kusoma, hata hivyo nilihairisha masomo hayo baada ya kuamua kuanza kuwa
mbunifu na mwaka 2013 nilizindua bidhaa yangu ya nywele na nguo
zijulikanazo kwa jina la ‘kidoti brand’ na sasa nimeingiza sokoni
kandambili aina ya kidoti,” alisema Jokate.
Alisema
kuwa alifanya utafiti wa kina ili kuteka soko la bidhaa zake na mpaka
sasa anazidi kubuni aina nyingine za mitindo ya nywele, nguo, kandambili
na bidhaa nyingine.
“Tusitegemee
ajira kutokana na kile tulichokisomea, tunatakiwa kuwa wabunifu na
kutumia vipaji vyetu, ukiweka nia tafanikiwa pamoja na ugumu wa kupata
mtaji na mambo mengine, kwa kufanya hivyo utaweza kumpa ajira mtu
aliyesoma zaidi yako, ipo mifano mingi duniani na matajiri wengi hawana
elimu ya kutosha, ila wamekuwa wabunifu na sasa wameajiri wataalam ambao
ni wasomi, hata hivyo soko la ajira ni dogo na wachache ndiyo
wanabahatika kupata kazi,” alisema.
Alisema
kuwa kwa sasa lengo lake kubwa ni kutawala soko na kuwa milionea pamoja
na kupata ushindani mkubwa katika soko kutokana na wingi wa bidhaa kama
zake.
0 comments:
Chapisha Maoni