Michuano
ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoshirikisha timu 27 inaanza
kutimua vumbi kesho (Mei 10 mwaka huu) katika vituo vitatu vya Morogoro,
Mbeya na Shinyanga kwa mechi mbili kila siku.
Kundi
A ambalo mechi zake zinachezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro,
African Sports ya Tanga itacheza na Kiluvya United FC ya Pwani saa 8
mchana wakati saa 10 jioni ni Mji Mkuu FC (CDA) ya Dodoma dhidi ya
Pachoto Shooting Stars ya Mtwara.
Jumapili
(Mei 11 mwaka huu) katika kundi hilo kutakuwa na mechi kati ya
Bulyanhulu FC (Shinyanga) na Kariakoo SC (Lindi) itakayoanza saa 8
mchana wakati saa 10 jioni ni Navy FC (Dar es Salaam) na Abajalo FC pia
ya Dar es Salaam.
Kundi
B katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya litaanza ligi kwa
mechi kati ya Ujenzi (Rukwa) na Volcano FC (Morogoro) saa 8 mchana
wakati saa 10 jioni ni AFC ya Arusha na Panone FC ya Kilimanjaro.
Mei
11 mwaka huu saa 8 mchana ni Mpanda United ya Katavi na Magereza ya
Iringa wakati Tanzanite (Manyara) na Njombe Mji (Njombe) zenyewe
zitaumana kuanzia saa 10 jioni.
Simiyu
United ya Simiyu na Mvuvumwa FC (Kigoma) ndizo zitakazoanza kucheza saa
8 mchana katika kundi C linalotumia Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga. Saa 10 jioni ni mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na mabingwa
wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars FC.
Jumapili
(Mei 11 mwaka huu), mechi za kundi hilo zitakuwa Singida United
(Singida) na Mbao FC ya Mwanza kuanzia saa 8 mchana wakati jioni ni
pambano kati ya mabingwa wa Mkoa wa Mara, JKT Rwamkoma FC na Geita
Veterans FC ya Geita.
Ligi
hiyo itamalizika Juni 2 mwaka huu ambapo timu itakayoongoza kila kundi
itapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015.
0 comments:
Chapisha Maoni