Maafisa wa Somalia wamekataa kukutana na maafisa wa
serikali ya Kenya na maafisa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la
kuwahudumia wakimbizi, ili kujadili mkataba uliofikiwa mwaka jana kuhusu
kuwarejesha kwao wakimbizi wasomali wanaoishi nchini humo.
Barua kutoka kwa waziri wa mambo ya nje wa
Somalia, ambayo BBC imeweza kuiona, inasema kuwa shughuli inayoendelea
ya kuwazuilia wakimbizi na kuwarejesha baadhi kwa nguvu Somalia,
inakiuka makubaliano hayo.Shirika la wakimbizi la Human Rights Watch linasema kuwa tangu mwezi jana maafisa wa Kenya wamekuwa wakiwakamata na kuwatesa wakimbizi wasomali na kuwarejesha baadhi yao kwa nguvu katika kambi za wakimbizi Kaskazini mwa Kenya.
Blogger Comment