Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amekabidhiwa leseni ya ngumi pamoja na kitambulisho na nyaraka mbalimbali za kumtambulisha kitaifa na kimataifa
Akizungumza wakati wa utoaji wa leseni kwa bondia huyo Rais wa shirika la ngumi za kulipwa nchini, Yassini Abdalla 'Ostadhi' amesema, leseni ni kitu ambacho kila bondia anatakiwa kuwa nacho ambapo inaweka kumbukumbu ya mapambano yote aliyocheza ndani na nje ya nchi.
"Hiki ni kitu muhimu sana leo hii natoa leseni kwa bondia Class kwa kuwa natambua kazi yake na uwezo wake akiwa katika uringo ambapo itamsaidia kwa ajili ya kazi yake kumbuka hii ni ajira hapa kajiajiri mwenyewe 'mtaji wa masikini nui nguvu zake mwenyewe'," alisema Yassin Abdalla
Nae bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' alishukuru kwa kusema leseni itamuongezea chachu ya kupigana vizuri zaidi awapo uringoni kwani ngumi ndio mchezo anao upenda na ndio anaucheza hivyo atafanya jitiada ili aweze kufika mbali kupitia mchezo wa ngumi
Bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha kutoka kambi ya Ilala likiongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' Kondo Nassoro, Sako Mtulya na Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye ana msimamia katika mapambano yake mbalimbali na kumpatia ushauri wa jinsi gani ya kupigana na watu anaokabiliana nao awapo uringoni
Via mwenda blog
0 comments:
Chapisha Maoni