
Emir wa Kano Al hajj Ado Bayero
Mazishi ya Emir wa eneo la KANO
kazkazini mwa Nigeria yamefanyika.
Al haji Ado Bayero mmoja wa viongozi wa kidini anayeheshimiwa sana nchini humo alifariki mapema siku ya ijumaa akiwa na umri wa miaka 83
Ni kiongozi wa pili kwa ukubwa wa dini ya kiislamu baada ya Sultan wa Sokoto.
Mwili wake ulizikwa katika makaburi ambayo mababu zake walizikwa karibu na nyumba yake huko Kano.
Kiongozi huyo wa dini alikuwa mkosoaji mkubwa wa kundi la wanamgambo wa boko haram.
Blogger Comment