Jeshi halijafika gwoza baada ya wiki 2

Ni wiki nane tangu wasichana 200 watekwe nyara kutoka shuleni mwao kazkazini mashariki mwa Nigeria.

Kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limeimarisha mashambulizi yake kufuatia milipuko ya mabomu katika miji kadhaa na vijiji.

Juma lililopita vijiji kadhaa vilivyoko karibu na mpaka na Cameroon vimeshambuliwa huku mamia ya raia wakiuawa.

Mwandishi wa BBC mjini Abuja amezungumza na baadhi ya raia ambao wamevitoroka vijiji katika eneo la Gwoza lililopo katika jimbo la Borno,na sasa wamejificha katika eneo la Milima la mandara karibu na mpaka wa Cameroon.

Wanasema kuwa juma moja baada ya shambulizi la wanamgambo wa boko haram hakuna ishara ya wanajeshi wa serikali katika eneo hilo.

Nyumba zao zilichomwa katika misururu ya mashambulizi ya wapiganaji hao ambayo yamesababisha mauaji ya mamia ya watu.

Kwa sasa wanalala hadharani katika maeneo ya milima hiyo.

Watu walioachwa bila makao wanasema kuwa wapiganaji wa Boko Haram wameweka bendara nyeupe na nyeusi za jihad katika vijiji kadhaa na kwamba ni hatari kwa raia kufika katika sehemu hizo.

Serikali ya Nigeria imeonekana kujivuta katika kukiri mashambulizi hayo huko Gwoza eneo ambalo sasa ni makao makuu ya Boko haram.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List