Kelele za baa, klabu kudhibitiwa

Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), imetunga kanuni ya kudhibiti kelele na mitetemo kutoka kwa waendeshaji wa klabu za usiku, baa, matangazo ya wanaozunguka barabarani na hata mahubiri katika maeneo ya ibada.

Kwa sasa kanuni hiyo iko kwa Mchapishaji Mkuu wa Serikali na tayari imesainiwa na Waziri anayeshughulikia Mazingira. Kadhalika wananchi wametakiwa kutoa taarifa za kero zitokanazo na maeneo hayo ya biashara kwani yamekuwa yakichangia kuporomosha maadili ya taifa.

Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji kutoka Baraza la Mazingira nchini (NEMC), Dk Robert Ntakamulenga alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia kero ambazo wananchi wamezifikisha ofisini kwake.

Malalamiko hayo yamekuwa yakielekezwa kwa Wizara ya Viwanda na Biashara ambao ndio wanaotoa leseni kwa ajili ya kuendesha biashara hizo. Wizara imesema haitotoa leseni nyingine za maeneo hayo ifikapo Julai.

Akizungumzia suala hilo, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, Dk Ntakamulenga alisema kero za kelele kutoka kwa wafanyabiashara hao zimekwua zikiwasumbua sana.

“Kutokana na kero hizo, ofisi ya makamu wa rais ikatunga kanuni kwa ajili ya kudhibiti uendeshaji wa biashara hiyo na atakayekiuka atachukuliwa hatua,” alisema Dk Ntakamulenga.

Alisema katika kanuni hiyo klabu za usiku, nyumba za ibada na baa zinatakiwa kufanyiwa tathmini ya athari ya mazingira kabla ya kupewa leseni ama kibali. Hata hivyo, alisema taratibu za uendeshaji wa biashara hizo zimekuwa zikivunjwa mara kwa mara kwani ni lazima ofisa kujiridhisha kabla ya kibali kutolewa.

Alisema NEMC katika suala la kelele, kuna viwango vya mijini, viwandani na vijiji na ni lazima kupata kibali kutoka halmashauri.

“Kama unapiga kelele inayozidi kiwango cha desbell 45 inahitajika kibali na kelele za aina hiyo ni zile zinazoanzia saa moja asubuhi hadi saa nne usiku iwe mwisho,” alisema na kuongeza baa ambazo zinapiga kelele za aina hiyo hadi usiku zinavunja sheria.

Kuhusu maeneo ya Ibada alisema kwa zile ambazo zinapiga kelele za aina hiyo zinatakiwa kuomba kibali na kwamba isizidi muda uliopangwa.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List