DR WILLBORD SLAA KWELI UMESHINDWA KUWATETEA WANANCHI WA TANZANIA SITA(6)TU CCBRT


Leo ni siku ya kesi  ambayo Vijana wa Tanzania wamefikishwa ndani ya mahakama ya Kazi(usuluhishi(CMA) kwa kosa la kugoma kufikia makubaliano ya kupunguzwa kazini kwa Vigezo vya kuwa na ELIMU ndogo kufanya kazi kitengo cha viungo Bandia CCBRT.Kesi hiyo ambayo imefunguliwa kwa kila mmoja CMA/DSM/R.258/KIN/14 namba ya kesi ya HENRY SHANGO JIMA na CMA/DSM/KIN/R.257/14 namba ya EDGAR TITUS LUGALA na washtikiwa wengine RASHIDI YAHYA SULTAN,RAMADHANI ABDALLAH,MAURICE RONDO na ASHA KIJORI.Kesi hiyo ipo chini ya JAJI Mh.CHENGULA jijini Dar Es Salaam

Mmoja wa mtumishi walioshtakiwa na CCBRT

Mmoja wa mtumishi walioshtakiwa na CCBRT
.
Vijana hao wameongea na vyombo vya habari juu ya kesi yao kwa kutoa malalamiko ya kutaka kufukuzwa kazi kinyemela kutokana na kubinifsishwa kwa kitengo hicho cha viungo bandia kisili.Pia wameshangazwa na taratibu ya kila mmoja kufunguliwa namba yake ya kesi wakati ni kesi moja.CCRBT ambao ni washtaki wa kesi hiyo wametumia kigezo cha Elimu kuwa ni Degree tu na sio DIPLOMA au Certificate kutokana na mahitaji ya mfadhili mpya NA viwango vya W.H.O(WORLD HEALTH ORGANIZATION) na I.S.P.O (International society for Prosthetics and Orthotics) ambapo pia vijana hao wakijibu wanasema'wao wanaye mtambua ni mwajili wao CCBRT na sio Mfadhili'

Kigezo hicho ambacho kimechukuliwa kama kikubwa kimepingwa vikali kutokana na Vijana hao kuajiliwa na kufanya kazi katika kitengo hicho kwa zaidi ya miaka mitano na Wengine wamefikisha zaidi ya Miaka kumi ndani ya kitengo hicho hivyo kwao ni kigezo ambacho hakina mshiko na Uonevu dhidi ya Wananchi wa Tanzania unaofanywa na Wageni toka nchi za nje.Pia kama Kigezo ni Elimu' kwa nini wasipatiwe Elimu na mwekezaji ili kuendeleza watanzania na si kuwatelekeza wafanya kazi wa ndani na kuwapa kipaumbele wageni toka nje'.

Mwisho wametoa malalamiko kwa bodi ya CCBRT(Comprehinsive Community Based Rehabilitation in Tanzania) kwa kufumbia macho na kushindwa kufanya jambo lolote kuwatetea ili kupata haki yao.Bodi ya CCBRT ambayo ipo chini ya Dr.Willbord Slaa imenyamazia suala hilo bila kutoa ushirikiano wowote kwa Vijana hao.

Picha ya mgonjwa anayepatiwa huduma na vijana hao waliofukuzwa kazi.
Hapa baada kuwekwa viungo bandia

      
baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa huduma ya viuongo bandia




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List