Diwani Sagamiko aandaa warsha kwa wenyeviti na makatibu UWT Kinondoni


Kuluthum Sagamiko akihojiwa na waandishi wa habari
mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo 


 Eva Mwingizi akihojiwa na waandishi wa habari mara
baada ya kufungua warsha hiyo.

  viongozi hao wakisikiliza watoa
mada (hawapo pichani) wakati wa warsha hiyo



DIWANI wa Viti Maalum Msasani, Kuluthum Sagamiko ameandaa warsha kwa ajili ya wenyeviti na makatibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya mafunzo ya kujiimarisha kichama na ujasiriamali
kwa wanawake.
Warsha hiyo ilifanyika Dar es salaam jana, ambapo jumla ya viongozi
hao kutoka kwenye kata 34 za wilaya hiyo walishiriki na kuweka
mikakati ya pamoja.  Akifungua warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu Bara, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Eva Mwingizi, aliwataka  kuwa mstari wa mbele na kusimama katika nyanja zote ikiwemo siasa na biashara bila woga.
Alisema uwiano sawa wa asilimia 50 kwa 50 katika uongozi hauwezi
kufikiwa endapo  wanawake wenyewe watasita kujitokeza kugombea nafasi
mbalimbali. "Nimefurahi leo kuwaona wanawake wamekutana pamoja, kwa sababu warsha kama hizi zinawajengea uwezo,kina mama wanaweza na wakijengewauwezo basi wanafanya vizuri katika nyanja zote.
"Kina mama ni mtaji mkubwa popote pale, ni tegemeo kwenye maeneo
mengi, hawa ni jeshi,ukitaka kufanikisha jambo, na kuwatumia kinamama
basi jambo hilo lazima lifanikiwe, kwahiyomafunzo ya kufanya
wajitambuezaidi ni muhimukwao,"aliongeza.
Alisema  ingawa UWT ipo kisiasalakini walifikiria kuwainua kina mama
kwa kuanzisha kitengo cha miradi, ambapopamoja namambomengine
kinawaunganisha na taasisi mbalimbali za mikopo ilikuinua biashara
zao. Naye muandaaji wa warsha hiyo, Diwani wa Viti Maalum Msasani, Kuluthum Sagamiko,alisema lengo ni kuwajengea uwezo wanawake  hao wanaotoka katika kata, kwakuwandiowenye watu .
"Pia wajitambue nakujipanga nachangamoto hususan  cha uchaguzi na
maisha kwa ujumla, hasa wakati huukuelekea katikachaguzi za
kitaifa,"aliongeza. Licha ya kupata mafunzo ya kisiasa,Kuluthum  alisema pia kunamkufunzi  wa mamboya biashara, ili kuleta msukumozaidi,kwa kuamini kuwa mwanamke mwenye uchumi ananguvu  zaidi.
"Kwenye wilaya yetuyaKinondoni, tumepoteza majimbo mawili na kata 11,
kupitia wanawake hawa, wenye nguvu nauelewa itakuwa rahisi kurudisha
maeneo tuliyopoteza kwa upinzani,"alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List