Suala la mimba za utotoni
na ndoa za utotoni imeonekana ni moja ya changamoto kwa wasichana
waliopo shule mblimbali hivyo wadau wa afya nchini wameshauriwa kubuni mbinu
mbadala za kutoa elimu ili kulikomboa kundi hilo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia kubainika kwa zaidi ya wasichana
8,000 kuwa na mimba kwa mwaka 2010 hali ambayo inatajwa kuzorotesha kiwango cha
Elimu kwa Wasichana.
Katika kukabiliana na tatizo hilo la wasichana shirika la
afya nchini la Marie Stoppes limesema ipo haja kwa Serikali pamoja asasi za
kiraia kuweza kukabiliana na hali hiyo.
Hata hivyo imebainika kuwepo kwa asilimia 16 tu ya elimu
madhubuti ya njia za kisasa za uzazi wa mpango kwa wasichana waliopo kwenye
ndoa hali ambayo inasababisha vifo vingi vya kundi hilo vitokanavyo na uzazi.
Kufuatia hali hiyo Marie Stoppes imebuni mkakati wa
kuwatembelea wanawake wajawazito kwa kutumia bajaji maalum yenye vifaa maalum
vitakavyosaidia kutoa elimu ya uzazi wa mpango.
Idadi ya vijana wa miaka kumi na 15 hadi 24 wanaotumia njia
za kisasa za uzazi wa mpango ni asilimia
16 tu ndo wana uwezo wakutumia kwa usahihi huku wengine wakiwa hawazielewi
kabisa njia hizo.
Hivyo njia hiyo itasaidia kutatua tatizo hilo ambapo mwaka
2010 kati ya hao 1,760 ni wanafunzi wa shule za msingi huku wa Sekondari wakiwa
6,300 na kuokoa kundi hilo.
Mwemezi Ngerema(Kaimu mkurugenzi Marie Stopes)
Wadau walioshiriki siku ya uzinduzi wa bajaji hizo maalum
Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Ilala
Mfadhiri wa Mradi wa bajaji maalum yenye vifaa maalum vitakavyosaidia kutoa elimu ya uzazi wa mpango.
Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Ilala na Mfadhili wa mradi wakizundua mradi.
Wadau walioshiriki siku ya uzinduzi wa bajaji hizo maalum.
bajaji maalum yenye vifaa maalum vitakavyosaidia kutoa elimu ya uzazi wa mpango.
Happines Watimanywa(miss Tanzania)
Wadau walioshiriki siku ya uzinduzi wa bajaji hizo maalum.
0 comments:
Chapisha Maoni