UVUMI WA KUPOTEA NA KUTEKWA KWA WATOTO WAWATIA HOFI WAZAZI WA WAILAYA YA TEMEKE

Hofu imetanda miongoni mwa wakazi wa jijini la Dar es salaam hususani wale wa jimbo la temeke kuhusu kuwepo kwa Taarifa za kutekwa kwa watoto wa kike na kiume wenye umri wa chini ya miaka sita.

Taarifa za kutekwa kwa watoto hao zimeanza kusikika takribani majuma matatu sasa,kwamba kuna kikundi cha watu wasiojulikana wanatumia gari aina ya Noah ama pikipiki kwa ajili ya utekaji huo.
Taarifa za kutekwa nyara kwa watoto hao zilianza kusambazwa maeneo ya Kigamboni,Mbagala hadi Yombo vituka jijini Dar es salaam ambapo watekaji wamedaiwa kuwapa watoto chipsi kuku kabla ya kufanya tukio la kuwateka.

Baada ya kusikia tetesi hizo mwandishi wa blog akaamua kufunga safari katika maeneo yote yaliyotajwa  kutekwa nyara kwa watoto.

Hakuna taarifa yoyote yenye kuthibitisha upotevu kwa watoto katika maeneo husika na wananchi wakashindwa kueleza ukweli wa jambo hilo kama ni kweli watoto wamepotea.Hiyo ikamfanya mwandishi afike hadi kwa KIHENYA KIHENYA(RPC TEMEKE).

Akiongea na Blog amesema kuwa huo ni uvumi lakini hakuna taarifa yoyote iliyopokelewa na vituo vya Polisi ya kutekwa kwa watoto na kuwaomba wazazi wasiwazuie watoto kwenda shule kwa kuhofia matukio hayo.
KIHENYA KIHENYA(RPC TEMEKE).

ANNA RAMADHANI mkazi wa Dar es salaam aliyedai mtoto kupotea lakini kaonekana.

STELLA ALPHONCE mkazi wa Dar es salaam aliyetoa maelezo juu ya utekwaji wa watoto.

 
MUSSA BARAKA akielezea uvumi huo wa kupotea kwa watoto.

Mtaa wa Yombo vituka kwa Alimboa ambapo kunadaiwa kupotea kwa watoto.

Mtaa wa Yombo vituka kwa Alimboa ambapo kunadaiwa kupotea kwa watoto.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List