Waathirika wa tukio la mabumu Mbagala wamemuomba Rais Jakaya
Kikwete kuwasaidia kupata fidia halisi ya Mali zao zilizopotea kutokana na
tukio hilo,kama alivyoahidi alipotembelea eneo hilo lilipotokea Aprili /29/2009 katika kambi ya Jeshi la
Wananchi JWTZ,KJ 0671 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20.
Baadhi ya familia zimeendelea kukosa mahala pa kuishi ,na
wengine wakiishi kwa ndugu,jamaa na marafiki,Huku mamia ya waliojeruhiwa
wakikosa mwelekeo wa kimaisha ,kutokana na kushindwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za uchumi.
Kwenye mkutano wao wa kujadili jinsi watakavyorudi kwa Rais
Kikwete ili kumshinikiza aingilie kati mchakato huo wa malipo,baada ya wengi
wao kulipwa viwango vidogo tofauti na mali zao zilizopotea.
Huku wakionyesha kwa masikito hundi hizo ambazo kuna baadhi
zinaonyesha hadi shiingi 1900,wananchi hawa wanahoji je?uhalali uko wapi kwenye
malipo ya viwango hivi.
Mwenyekiti wa Waathirika wa mabomu Ndugu Steven Gimonge ametoa malalamiko yake dhidi ya
watumishi waliohusika na zoezi la tathimini kuwa walikuwa sio waaminifu,hali iliyosababisha
malipo ya fidia kufikia viwangi hivyo.
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Faustin Ndungulile amekiri kuwepo
kwa tatizo hilo,huku akiwataka kushirikiana nae katika kuhakikisha haki zao
zinapatikana.Hata hivyo wametakiwa kuendelea kuwa wavumilivu wakati ambapo
Serikali inaendelea kulitafutia ufumbuzi jambo hilo,Ingawa wananchi wenyewe
wanaonyesha kuchoshwa na ahadi hizo za mara kwa mara zisizotekekelezeka.
Baadhi ya majengo yaliyo haribika na Mabumu ya Mbagala.
Baadhi ya majengo yaliyo haribika na Mabumu ya Mbagala.
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Faustin Ndungulile
Mmoja wa waathirika wa Mabomu ya Mbagala wanaodai fidia.
Baadhi ya majengo yaliyo haribika na Mabumu ya Mbagala.
Mmoja wa waathirika wa Mabomu ya Mbagala wanaodai fidia.
Baadhi ya majengo yaliyo haribika na Mabumu ya Mbagala.
Mwananchi aliyepoteza uwezo wa kuona kutokana na Mlipuko wa mabomu ya Mbagala.
Mmoja wa waathirika akionyesha malipo ya fidia kiduchu.
Mwenyekiti wa waathirika wa Mabomu Ndugu Steven Gimonge
Wananchi ambao wanalalamikia malipo kiduchu wakiwa katika mkutano.
0 comments:
Chapisha Maoni