Rais wa Tanzania Mh:JAKAYA MRISHO KIKWETE azindua barabara ya Mwenge hadi Tegeta

Rais Dk  Jakaya Mrisho Kikwete amesema Serikali imeanza kukabiliana na Tatizo la msongamano wa Magari kwa kujenga barabara nyingi zaidi ikiwa ni pamoja na kuongeza miundombinu mipya ya njia za reli na vyombo vya Majini  hususani za maeneo ya mijini.

Akizindua barabara ya Mwenge hadi Tegeta yenye urefu wa kilometa 12.9. Dk Kikwete amesema hatua hiyo itaenda sambamba na mpango wa Serikali kuanza kusajili mabasi yatakayotumika kubeba abiria yawe ya viwango vya kuridhisha.


Akikata Utepe katika uzinduzi wa barabara hiyo, Dk. kikwete amesema, Tatizo la msongamano wa magari si la Tanzania pekee bali ni la dunia nzima, na moja ya njia ya kukabiliana nalo ni  kuwa na mabasi mazuri yatakayowashawishi watu kuyatumia na kuacha magari binafsi nyumbani.


Barabara hiyo iliyogharimu shilingi bilioni 99.6 imefadhiliwa na serikali ya Japan kupitia shirika lake la maendeleo-JICA, ndiyo itakayotumiwa kwa mabasi yote ya abiria yaendayo mikoa ya kaskazini.

Mara nyingi penye Barabara nzuri ndipo ajali zinaongezeka na katika hilo rais kikwete anasema hivi sasa hali inatisha kwani idadi ya vifo kwa ajili ya pikipiki vimekuwa vingi kuliko idadi ya vifo vya ugonjwa

Uzinduzi hup ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo balozi wa japan,mkuu wa mkoa wa dar es salaa,mbunge wa jimbo la Kawe, mkurugenzi wa tanroad

Kwa mujibu wa rais kikwete serikali pia inakusudia kuanzisha usafiri wa mijini kupitia bahari ambapo pia akaweka wazi mpango uliopo wa kujenga barabara za juu katika barabara za makutano.

Mh:JAKAYA MRISHO KIKWETE RAIS WA TANZANIA akihutubia wananchi.


Mh:JAKAYA MRISHO KIKWETE akisindikizwa na baadhi ya viongozi baada ya kuwasili.

Viongozi mbalimbali wakijiandaa kumpokea Mh:JAKAYA MRISHO KIKWETE akiwasili maeneo ya uzinduzi.

Mh:JAKAYA MRISHO KIKWETE(Rais wa Tanzania)akiweka jiwe la msingi siku ya uzinduzi wa barabara.

Mh:JAKAYA MRISHO KIKWETE(Rais wa Tanzania)akizindua barabara

Mh:JAKAYA MRISHO KIKWETE(Rais wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja)

Mbunge wa Jimbo la kawe Mh:Halima Mdee akiwa anafuatilia uzinduzi wa barabara hiyo.

Mh:JAKAYA MRISHO KIKWETE(Rais wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja)

Waannchi wakifuatilia ufumbuzi wa barabara 

Kikundi cha utamaduni kilichotumbuitiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa Barabara


Mh:JAKAYA MRISHO KIKWETE(Rais wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja)

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List