Wazee wa chama cha mapinduzi wametakiwa kuwa chachu ya
upatikanaji wa viongozi mahiri wa chama kwenye ngazi mbalimbali,watakaoweza
kwenda sambamba na sheria na kanuni za chama zilizowekwa na Muasisi wa
Chama,Hayati Baba wa taifa Mwalimu
Julius Nyerere.
Hayo yamesemwa kwenye mkutano wa wazee kupitia jumuiya ya
wazazi kata ya Mwijuma na Makumbusho wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
salaam,baada ya kubainika kwamba maeneo
mengi yanachukuliwa na wapinzani baada ya viongozi wa chama hicho kushindwa
kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha.
Mwenyekiti wa Ccm wilaya ya kinondoni Salum Madenge amesema
Chama cha Mapinduzi Kinawategemea zaidi wazee katika kuhakikisha Chama kinapata
viongozi bora na wenye Busara.
Mwenyekiti wa UWT kata ya Makumbusho Salama Chalembo
amewakumbusha kuwa huu ni wakati wa kurudisha heshima ya chama,hasa
wanapoelekea uchaguzi mkuu.
Baadhi ya wazee wa Jumuiya ya Wazazi kupitia Chama cha
Mapinduzi waliohudhulia mkutano huo walizungumzia namna ya kutatua changamoto
zilizopo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya kinondoni Mh:SALUM MADENGE
Mwenyekiti wa wazazi kata ya Makumbusho Mh:SAID ABDALAH SUBETY
Mjumbe wa Mkutano wa wazazi akitoa mawazo
Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Makumbusho akihamasisha wazazi katika mkutano.
Baadhi ya Viongozi wa CCM kata ya Makumbusho.
Wanachama wa CCM wa jumuiya ya Wazazi wakifuatilia kwa makini.
Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Makumbusho akihamasisha wazazi katika mkutano.
Baadhi ya Viongozi wa CCM kata ya Makumbusho.
Wanachama wa CCM wa jumuiya ya Wazazi wakifuatilia kwa makini.
0 comments:
Chapisha Maoni