Taasisi za elimu kunyimwa fursa za kuandika Vitabu vya Kiada,vitakavyoweza kutumika kwenye shule za
msingi na sekondari,kunatajwa kama miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia
ongezeko la kuporomoka kwa kiwango cha elimu nchini.
Kumekuwepo na tofauti kubwa ya viwango vya utoaji wa elimu
wa ,huku moja ya sababu zake ikiwa ni tofauti ya uandikaji wa vitabu
,unaofanywa kwa kiasi kikubwa na waandishi
binafsi.
Mkurugenzi wa shule ya Sekondary ya Madiba Joel Kajula amesema ipo haja kwa Wizara
ya elimu kuliangalia upya suala la
kuziachia taasisi za elimu kuandika
Vitabu vinavyotumika kwenye mitaala ya Tanzania ,ili kutengeneza usawa
kwenye utoaji wa elimu.
Mgeni rasmi kwenye mahafali haya ya nane secondary ya Madiba
pia ikitimiza miaka kumi Dr Zacharia Kanyeka Mhadhiri mwandamizi UDSM amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na
kuachana na njia za mkato katika kutafuta elimu bora .
Baadhi ya wazazi waliohudhuria mahafari hayo pamoja na
wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne Madiba wamezungumzia siri ya mafanikio ya
shule hiyo.
Jumla ya wahitimu 39 wa kidato cha nne wavulana 18 na
wasichana 21 wamehitimu kwenye Mahafali hayo ya 8 sekondary ya Madiba huku
ikifikia miaka kumi tokaianzishwe huku ikiwa inarekodi ya kufanya vizuri.
wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya Sekondary ya Madiba
Mgeni rasmi Dr.ZACHARIA KANYEKA(Mhadhiri mwandamizi-UDSM)
Ndugu:JOEL KAJULA Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya Madiba
Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondary ya Madiba.
Meza kuu siku ya mahafali kidato cha nne shule ya Sekondary ya Madiba.
ndugu,BERDARD KINDOLI(mwenyekiti wa kamati ya shule)
Wazazi waliokuja kuudhulia mahafali ya kidato cha nne ya shule ya Sekondary ya Madiba.
Wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne ndani ya shule ya Sekondary ya Madiba.
Wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne ndani ya shule ya Sekondary ya Madiba.
Mmoja wa wazazi akitoa zawadi kwa Mwalimu Mkuu.
Wanafunzi waliowahi kumaliza ndani ya shule ya Sekondary ya Madiba
Wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne ndani ya shule ya Sekondary ya Madiba wakiimba kwaya.
Majengo ya shule ya Sekondary ya Madiba
0 comments:
Chapisha Maoni