Mamlaka ya mapato nchini TRA imekabidhi vifaa
mbalimbali kwa hospitali kuu ya mnazi mmoja iliyopo wilaya ya mjini hapa
Zanzibar
Akikabidhi msaada huo kwa uongozi wa Hospitali hiyo Richard M
Kayombo mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi amesema TRA kila mwaka
imekuwa ikitoa misaada katika maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na magodoro 100,shuka 100,pashet
screen 10 na oxygen set 3 ambapo vifaa vyote vimegharimu jumla ya shilingi
milioni 20
Akipokea vifaa hivyo Dr Msafiri Marijani mkuu wa idara ya
uchunguzi katika hospitali ya hiyo ameishukuru TRA kwa msaada huo na kusema
kuwa hospitali hiyo bado ina changamoto nyingi kutokana na ufinyu wa bajeti,na
kuziomba taasisi nyengine kuiga mfano wa TRA.
Aidha Kayombo amefahamisha kuwa mwaka huu wa 2014 TRA inafanya
maadhimisho ya nane na tayari wamekabidhi madawati kwa shule kadhaa jijini
Dar es Salaam na kushiriki usafi katika hospitali ya Wilaya ya Temeke.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo Mkurugenzi
wa huduma na elimu kwa mlipa kodi TRA makao makuu amesema TRAnchini ilianza
rasmi mwaka 1996 ambapo kwa kipindi hicho makusanyo ya mwaka yalikuwa shilingi
bilioni 35 na makusanyo yamefikia kiasi cha shilingi bilioni 900 kwa mwaka wa
2013/14.
Mkurugenzi huyo pia amewataka wafanyabiashara na wananchi wote
nchini kuzingatia kulipa kodi ili kuinua uchumi wa taifa,pia amewataka
watumiaji wa bidhaa kudai risiti ili kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hawakwepi
kodi.
Kilele cha wiki ya mlipa kodi kitafikiwa siku ya tarehe ambapo
wafanyabiashara wanaolipa kodi bila shuruti watatangazwa hadharani na
kutunukiwa vyeti maalumu na TRA.
0 comments:
Chapisha Maoni