Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeizuia timu ya Polisi Mara kutumia
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma kwa mechi zake za Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia leo mpaka hapo itakapotangazwa
vinginevyo.
Uamuzi
huo umechukuliwa kutokana na matukio ya vurugu na uvunjifu wa amani
ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mechi za FDL zinazochezwa kwenye uwanja
huo, ikiwemo ile ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Mwadui ya Shinyanga
ambapo waamuzi walipigwa.
Kamati
zinazohusika zitakutakana hivi karibuni kupitia matukio yote ya utovu
wa nidhamu kwenye FDL, na hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika ikiwemo
na viwanja ambavyo vimekuwa na sifa ya vurugu.
Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vina wajibu wa kutoa ulinzi wa kutosha viwanjani wakati wa mechi.
RAUNDI YA PILI TAIFA CUP WANAWAKE JUMAMOSI
Mechi
za kwanza za raundi ya pili ya mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu
kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake) zinachezwa wikiendi hii (Januari 17
mwaka huu) kwenye miji minane tofauti nchini.
Timu
tisa zilizofuzu kutoka raundi ya kwanza baada ya mechi za nyumbani na
ugenini akiwemo mshindwa bora (best loser) zitaungana na Ilala,
Kinondoni na Temeke kucheza raundi ya pili. Mechi za marudiano za raundi
hiyo zitachezwa Januari 21 mwaka huu.
Hatua
ya robo fainali itakayochezwa Januari 26 na 27 mwaka huu pamoja na nusu
fainali na fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Proin Promotions
itafanyikia jijini Dar es Salaam.
KOCHA NOOIJ KUTAJA STARS MABORESHO
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij anatarajia kutaja kikosi cha Maboresho
kitakachoingia kambini Januari 18 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya
kirafiki dhidi ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu jijini
Mwanza.
Nooij
atataja kikosi hicho kwenye mkutano na waandishi wa habari
utakaofanyika kesho (Januari 15 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume.
RAMBIRAMBI MSIBA WA STEPHEN NSOLO
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya
msiba wa Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Shinyanga (SHIREFA) uliotokea jana (Januari 13 mwaka huu) jijini Mwanza.
Msiba
huo ni pigo kwa wadau wa mpira wa mpira wa miguu kwani wakati wa uhai
wake, Nsolo alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi. Aliongoza SHIREFA
akiwa Katibu kuanzia mwaka 1975 hadi 1994.
Kabla
ya hapo alikuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga
kwa kipindi cha miaka kumi. Pia aliwahi kuwa mwamuzi wa daraja la kwanza
na kamishna wa mpira wa miguu kwa muda mrefu.
TFF
inatoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, SHIREFA na Chama
cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na kuwataka kuwa na subira
na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwa msiba huo.
Marehemu
anatarajiwa kuzikwa leo (Januari 14 mwaka huu) katika makaburi ya
Shinyanga Mjini. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Chapisha Maoni