Waziri WA fedha Saada afanya ziara ya kushtukiza Kariakoo na Mtaa wa Namanga

 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kulia) akiongoza na viongozi wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na maafisa wa Serikali alipofanya ziara ya kushtukiza leo jijini Dar es salaam katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. Wa kwanza kulia ni Kaimu Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA Hamidu Athmani, wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala Elias Balongo na kushoto mwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof.  Adolf Mkenda.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kushoto) katika ziara ya kushtukiza katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. Aliyevaa tai kulia ni wa kwanza kulia ni Kaimu Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA Hamidu Athmani.
. Wananchi wakifuatilia ziara ya kushtukiza ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum aliyofanya leo jijini Dar es salaam katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini.
(Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List