Chid Benzi Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwili Jela au Kulipa Faini ya sh. 900,000




Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa hayo.


Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.

Hata  hivyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo   imemwachia huru mwanamuziki huyo  baada ya kulipa faini ya 900,000/
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List