Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer), Ahmed Mgoyi kwa ushindi wa jumla wa mabao 12- 9 dhidi ya timu ya Taifa kutoka nchini Kenya.
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, mwishoni mwa wiki iliibuka na ushindi wa mabao 7-6 katika mchezo uliofanyika kwenye Ufukwe wa klabu ya Escape 1 eneo la Msasani Jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake Bw. Malinzi amesema ushindi walioupata timu ya soka la Ufukweni mwishoni mwa wiki, umeitangaza vizuri nchi ya Tanzania na kuwataka Viongozi wa soka la Ufukweni, makocha, wachezaji kutobweteka na ushndi huo, zaidi kujipanga kwa maandalizi ya mchezo utakaofuata.
Baada ya kuitoa timu ya Taifa ya Kenya, Tanzania watacheza na timu ya Taifa ya Misri mapema mwezi ujao ambapo mchezo wa awali utafanyika jijini Dar es salaam kati ya mwezi Machi 7, 8 na marudiano kufanyika baada ya wiki moja nchini Misri.
Endapo timu ya Taifa ya Tanzania itaiondoa timu ya Taifa ya Misri, moja kwa moja itakata tiketi ya kushiriki Fainali za Mataifa Afrika kwa Soka la Ufukweni 2015 zinazotarajiwa kufanyika Visiwa vya Shelisheli kuanzia April 14 - 19 mwaka huu.
Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Ufukweni kwa ushindi huo na kuwatakia maandalizi mema kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Misri.
0 comments:
Chapisha Maoni