Je CHADEMA wana zingatia Demokrasia kwa Maamuzi ya Kumtoa Zitto Kabwe Uanachama.

Mwanasheria mkuu wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.

"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwa hiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema"

Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.

Licha ya kutupilia mbali kesi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, Mahakama kuu imemtaka kulipa gharama zote za kesi toka ilivyoanza.

Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili na hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List