NGUMI KUFANYIKA MKWAKWANI TANGA MEI 2

Bondia Alen Kamote wa Tanga atapanda uringoni mei 2 katika uwanja wa mkwakwani tanga kukabiliana na Emilio Norfat katika mpambano wa raundi 12 mbali na mpambano uho siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine makala moja ya mpambano wenye mvuto zaidi ni kati ya bondia mwenye makazi yake mkoa wa Morogoro Cosmas Cheka atakaekabiliana na Said Mundi kutoa mkoa wa tanga
 
promota wa mpambano uho Ally Mwazoa aliongeza kwa kusema mbali na mapambano hayo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha  Jacobo Maganga na Fadhili Kea wakati Juma Mustafa akipamana na Ally Magoma uku Saimon Zabroni akioneshana umwamba na Hamisi Mwakinyo
na Jumanne Mohamed na Bakari Shendekwa na Zuber Kitandura na Rajabu Mahoja

mpambano uho unafanyika mkoa wa tanga baada ya kutopata burudani ya mchezo wa masumbwi kwa kipindi cha mda mrefu kidongo hivyo mpambano uho utafuraiwa na wakati wa Tanga na vitongoji vyake

siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List