ALLY BAKARI CHAMPION ACHUKUWA JIKO



Refarii wa mchezo wa masumbwi nchni kushoto akiwa na mke wake Aisha Chilumba  baada ya kuowa hivi karibuni maendeo ya Vingunguti Dar es salaam


Refarii wa mchezo wa masumbwi nchni kushoto akiwa na mke wake Aisha Chilumba  baada ya kuowa hivi karibuni maendeo ya Vingunguti Dar es salaam

BALOZI MISS KILIMANJARO KUTAFUTWA MWEZI UJAO KATIKA UKUMBI WA KILI HOME RESORT


Baadhi ya warembo watakawo wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika julay 24 katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshi wakiwa katika pozi wakati wa utambulisho wa mashindano hayo
Baadhi ya warembo watakawo wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika julay 24 katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshi wakiwa katika pozi wakati wa utambulisho wa mashindano hayo

Mlatibu wa mashindano ya urembo ya Kilimanjaro Ambassador Jacqueline Chuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchuano huo utakaofanyika katika ukumb wa Kili Home Resort

BANZA STONE AZUSHIWA KIFO,ASHA BARAKA AKANUSHA

UZUSHI wa kifo cha mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi nchini Ramadhani Masanja Banzastone wawapa mashabiki wa muziki wake taharuki usiku wa jana huku mwajiri wake wa zamani Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka akikanusha vikali kwamba habari hizo zilizozagaa jana usiku ni za uongo.

Akizungumza leo asubuhi kwa njia ya simu Asha alisema kwamba "Huo ni uzushi wa kwenye mitandao Banzastone yu hai licha ya kwamba ana umwa" alisema Asha.


Hivi karibuni iliripotiwa na vyombo vya habari kwamba hali ya mwanamuziki huyo kuwa siyo nzuri kiasi kwamba amegoma kula huku mama yake mzazi akilalamika kwamba wasanii wenzake hawaonekani kumsaidia hivyo anaomba msaada wa hali na mali.

Wakati huohuo mtandao wa Saluti5 unaripoti kuwa Habari hizi si za kweli na ni uzushi wa kipuuzi. Saluti5 imepokea zaidi ya simu 15 zikitaka uthibitisho juu ya habari hizo ambazo sasa zimekuwa kama mazoea juu ya msanii huyo. 

Hii ni zaidi ya mara 10 Banza anazushiwa kifo. Banza Stone yu hai na anaendelea vizuri, Saluti5 imeongea na amesema anashukuru mungu hajambo.

Tuesday, June 23, 2015

WASAMBAZAJI WA FILAMU KUGOMA KULIPA KODI IFIKAPO JULAY MOSI

Mwenyekiti wa chama cha wasambazaji wa Filam TAnzania 'TAFDA' Moses Mwanyilu kushoto akionesho moja ya filamu  kwa wahandishi wa habari katika ukumbi wa Idara Habari Maelezo Dar es salaa  awapo pichana juu ya filamu ambazo zinauzwa kiolela bila ya kulipa kodi tena kwa galam nafuu kulinganisha na zao ambao wanalipa kodi kupitia mamlaka ya Mapato TRA  ambapo julay mosi wameazimia kuto peleka filamu zao bodi ya filamu na kutonunua stemp kwa ajili ya ulipaji wa kodi wa pili kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa chama hico Suleiman Ling'ande

 
 Mjumbe wa chama cha usambazaji wa Filamu nchini Saleh Abdallah kushoto akizungumza na wahandishi wa habari awapo pichani juu ya filamu zilizojaa mtaani ambazo azijalipiwa kodi uku zikiachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote ile wakati wao filamu zao zinakaguliwa na Bodi pamoja na kulipa kodi katika mamlaka ya mapato TRA kulia ni Mwenyekiti wa chama cha wasambazaji wa Filam TAnzania 'TAFDA' Moses Mwanyilu



 Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania,Bw Moses Mwanyilu akionyesha baadhi ya filamu ambazo zinauzwa nchini bila kupata kibali kutoka bodi ya filamu Tanzania na kutokuwa na stika za ushuru za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakielezea changamoto zao kuhusiana na filamu za kitanzania kulazimishwa kukaguliwa na bodi ya filamu na kuwekwa stika za TRA ilhali filamu za nje hazifanyiwi hivyo na kupelekea filamu za kitanzania kutokuwa na ushindani sokoni.


Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania,Bw Moses Mwanyilu akionyesha filamu kutoka nje ambayo inasemekana kuwa na maadili yasiofahaa kutazamwa na watoto chini ya miaka 18 ambayo inaendelea kuuzwa nchini huku ikiwa haijakaguliwa na bodi ya filamu wala haina stika za TRa kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza watayarishaji na wauzaji wa filamu za kitanzania ambazo zimekuwa na mlolongo mrefu hadi kuingia sokoni.


 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kuandika kile kinachozungumzwa 

Mjumbe wa chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Saleh Abdallah akizungumzia kauli moja waliyokubaliana kama wasambazaji kuwa Kuanzia tarehe 1 Julai 2015 wao kama watayarishaji na wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania wamesitisha swala la kupeleka filamu zao bodi ya filamu kwaajili ya kukaguliwa wala kununua stika za TRA mpaka pale mamlaka husika zitakapokaa chini na kujadiliana kuhusu swala hili

Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao bodi ya filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu 

Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya filamu ya mwaka 2012 ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja.

Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka filamu sokoni.

Saturday, June 20, 2015

BENKI YA CRDB YAKABIDHI PASSO KWA MSHINDI WA SHINDANO LA 'Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo'

Mshindi wa Promosheni ya 'Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo' Mwinyi Khamis Juma mkazi wa Mbalali mkoani Mbeya, akipunga mkono baada ya kukabidhiwa zawadi yake katika hafla iliyofanyika mkoani Mbeya juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoa wa Mbeya, Benson Mwakyusa na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa. (Na Mpiga Picha Wetu) 

Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (aliyeshika mfano wa ufunguo) akizungumza neno muda mfupi kabla ya makabidhiano wa zawadi ya Passo kwa mshindi wa Mkoa wa Mbeya, Mwinyi Khamis Juma. Kushoto ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Mwanjelwa, Ephraim Lwila na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Sumbawanga, Colnerius Msigwa (kulia) 
 Mshindi wa Shindano la "Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo" Mwinyi Khamis Juma mkazi wa Mbalali mkoani Mbeya, kiushukuru uongozi wa Benki ya CRDB baada ya kuibuka mshindi wa Promosheni ya Shindano la 'Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo' inayoendeshwa na benki ya CRDB. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Mwanjelwa, Ephraim Lwila. 

Monday, June 15, 2015

BM HAIR & BEAUTY CLINIC WAZINDUA HUDUMA MPYA JIJINI DAR


 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akikata utepe kuzindua huduma mpya za BM Hair and Beauty Clinic huku akisaidiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele leo jijini Dar es Salaam. Kwa sasa wamefikisha miaka 14 kwa kutoa huduma zenye ubora tokea imeanzishwa.  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akionyesha grasi juu yenye kinywaji pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele kuashiria kuzinduliwa kwa huduma mpya.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimia na wafanyakazi wa BM Hair and Beauty Clinic mara baada ya kuzindua huduma za kipekee ijulikanayo kwa jina la (Premier Services) iliyofanyika Kinondoni jijini Dar es Salaam. Pembeni kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele.
Mmoja ya wafanyakazi wa BM Hair & Beauty Clinic, Neema Mushi akimpa maelezo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda juu ya huduma wanazozitoa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele akimpa maelezo machache Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda juu ya bidhaa na huduma wanazotoa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akionyeshwa na kupewa maelezo juu vifaa mbali mbali vya kisasa vinavyopatikana ndani ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele.
Tukizungumzia suala la vifaa vyenye ubora BM Hair & Beauty Clinic inaongoza na sasa imeongeza huduma zake.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiondoka eneo la tukio mara baada ya kumaliza kuzindua huduma mpya za BM Hair & Beauty Clinic.
Wafanyakazi wa BM Hair & Beauty Clinic wakishangilia mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele na wafanyakazi wa BM Hair & Beauty Clini

MFANYABIASHARA JUMA RAIBU ATANGAZA NIA KUGOMBEA UDIWANI KATA YA PASUA MJINI MOSHI.


Umati mkubwa wa wanachi katika kata ya Pasua wakilmsikiliza mfanyabiashara Juma Raibu (hayupo pichani wakati akitangaza nia ya kuwania nafasi ya Udiwani katika kata ya Pasua.

Mfanyabiashara Juma Raibu akifutilia kwa makini wahutibiaji wa awali wakati wa mkutano wa hadhara ambao uliandaliwa kwa ajili ya kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Udiwani katika kata ya Pasua.
Baadhi ya wananchi waliohudhulia mkutano huo.
Baadhi ya wananchama wa vyama vya upinzani waliojitokeza kurudisha fomu wakati wa mkutano huo.
Mfanyabiashara Juma Raibu (aliyevalia shati la kijana )akizungumza na watu waliomsindikiza mara baada ya kurejea nyubani kwake mara baada ya kumalizika kwa mkutai wa hadhara ambao aliutumia kutangaza nia ya kugombea nafasi ya udiwani katika kata ya Pasua mjini Moshi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kskazini.

NASSAR AISHUKURU BENKI YA NMB KWA MISAADA INAYOENDELEA KUTOA KWA WANANCHI KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI.

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akifurahia msaada wa madawati toka Benki ya NMB ,wengine ni viongozi kutoka katika benki hiyo pamoja na viongozi waliokuwa wakiiwakilisha serikali. 
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Usa River,Bernadeta Mmary akikabidhi msaada wa madawati kwa mwakilishi wa afisa elimu ,Jumanne Masuke uliotolewa na benki kwa shule ya msingi ,Sura iliyopo kijiji cha Songoro wilayani Arumeru.
Mbunge Joshua Nassar akizungumza wakati wa hafla fuoi ya kukabidhi msaada wa madawati uliotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya shule ya msingi Sura iliyopo kijiji cha Songoro wilaya ya Arumeru.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameketi katika madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB.
Baadhi ya wazazi wenye watoto katika shule ya msingi Sura iliyopatiwa msaada wamadawati na Benki ya NMB.
Meneja wa NMB tawi la Usa River ,Bernadeta Mmary akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo wa madawati.
Makilishi wa Afisa elimu wa wilaya ya Meru,Jumanne Masuke akizungumza katika hafla hiyo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Sura ,Raphael Akyoo akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa madawati.
Mwakilishi wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini ,Helen Binarita akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika shuleni hapo.
Mbunge Nassar pamoja na viongozi wa benki ya NMB wakiwa katika picha ya pamojamara baada ya kukabidhi msaada wa madawati.
Moja ya darasa katika shule ya msingi Sura likiwa halina madawati.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List