BANZA STONE HAFARIKI DUNIA

MWANAMUZIKI mkongwe nchini Ramadhani Masanja ‘Banzastone’ amefariki dunia nyumbani kwao Sinza njia panda Lion jana mchana baada ya salat Jumaa.

Banzastone amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu  huku akipelekwa hospitali na kutibiwa nyumbani kwa tiba za aina mbalimbali.

Taarifa rasmi za kifo cha mwanamuziki huyo zilitolewa jana na kaka yake Khamis Masanja .
Masanja alisema kwamba  kifo cha Banzastoner kimekuja baada ya kuugua kwa muda mrefu ambapo alikuwa akisumbuliwa na kifua pamoja na fangas za kichwani.
Aidha kaka huyo wa marehemu alisema kwamba taratibu za mazishi zinafanyika kwa kuzingatia familia yao ilivyokua kubwa  hivyo taarifa zaidi zitatolewa hapo baadaye.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List