Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mpinduzi (UVCCM) mkoani Arusha amezuiwa kuingia ofisini leo asubuhi na baadhi ya makada wa chama hicho kufuatia tuhuma zinazomkabili za kughushi nyaraka za Usalama wa Taifa na kufanyia utapeli.
Makada wa chama hicho walifunga ofisi hizo mapema leo alfajiri wakisema kuwa mwenyekiti huyo, Lengai Ole Sabaya hana hadhi tena ya kuwa mwenyekiti wa umoja huo mkoani Arusha baada ya kughushi nyaraka za Idara ya Usalama wa Taifa kufanya utapeli.
Lengai Ole Sabaya, Mwenyekiti wa UVCCM Arusha.
Baadhi ya makada ambao ni watiifu kwa mwenyekiti huyo wameonekana
wakimsaidia aweze kuingia ofisini wakijitahidi kuwaondoa waliokuwa
wakimzuia bila mafanikio.
0 comments:
Chapisha Maoni