Magufuli awatunuku kamisheni maafisa 205 wa jeshi

RAIS, Dk .John Magufuli leo amewatunuku Kamisheni kwa Cheo cha Luteni Usu, Maafisa Wanafunzi Wapya 205 pamoja na kutoa Nishani kwa Maafisa watano waliofanya vizuri kwenye masomo yao.

RAIS, Dk .John Magufuli leo amewatunuku
Kamisheni kwa Cheo cha Luteni Usu, Maafisa
Wanafunzi Wapya 205 pamoja na kutoa Nishani
kwa Maafisa watano waliofanya vizuri kwenye
masomo yao.
Rais alitoa Kamisheni hiyo kwa Cheo cha Luteni
Usu leo, katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi
Monduli (TMA) ikiwa ni mara yake ya kwanza
tangu akiwa Rais.
Miongoni mwa Maafisa hao wapya watano
waliotunukiwa nishani zao ni wanawake wawili
ambao ni Efrasia Bundala kutoka Tanzania na
Winnie Indumuli kutoka nchini (Kenya) huku
wanaume wakiwa watatu ambao ni Phinias
Kiganga aliyefanya vyema darasani.
Wengine ni Frank Kitalekwa aliyefanya vyema
upande wa medani na Ahmed Mmang'anda
aliyefanya vyema darasani.
Baada ya kuwavisha nishani askari hao watano
ambao ni miongoni mwa maafisa wapya 205,
Rais Magufuli aliwatunuku Kamisheni kwa cheo
cha Luteni Usu maafisa hao wapya ambao
miongoni mwao wanawake ni 16 na wanaume
wakiwa 189.
Aidha miongoni mwa wahitimu hao wawili
wanatoka nchini Burundi, 4 nchini Kenya na 4
wanatoka nchini Uganda ambao ni nchi marafiki.
Mara baada ya kutoa kamisheni kwa maafisa
hao, Rais Magufuli alipata burudani kutoka kwa
Kikundi cha Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Oljoro
ambao walipokuwa wakiimba walimpongeza Rais
Magufuli kwa utendaji wake wa kazi na
kumuomba kusafisha wabadhirifu wote wakwepa
kodi pia asafishe taasisi mbalimbali ili Tanzania
iwe safi.
Nayo bendi ya Jeshi la Watanzania(JWTZ)
iitwayo Chacharika Bendi ilikonga nyoyo za
wananchi waliofurika kushuhudia ndugu zao
waliotunukiwa Kamisheni zao huku
wakimpongeza kwa utoaji wa elimu bure.
Pia alipiga picha na maafisa hao wapya, viongozi
mbalimbali.
Awali akiingia uwanjani kwa ajili ya ukaguzi wa
gwaride Rais Magufuli alishangiliwa na wananchi
mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo lakini pia
viongozi wa serikali pamoja na wageni waalikwa
waliohudhuria katika sherehe hiyo.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List