Shule ya Msingi Jeshi la wokovu ya jijini Dar es salaam,inayotoa Elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum,ina upungufu wa walimu wa Sayansi na hisabati kwa muda mrefu hivyo imeiomba serikali kuwasaidia watoto wenye uhitaji ili wapate elimu.
Hayo yamesemwa wakati wa kupokea msaada wa Baiskeli na Fimbo kwa watoto wenye ulemavu wa macho na miguu Kutoka kwa taasisi ya Mohamed Punjan Foundation ya nchini CANADA.
Meja Wilson Chacha ni Mkurugenzi wa shule ya Jeshi la wakovu ameshukuru msaada huo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaosoma katika shule hiyo huku wazazi wao wakiwa hawana uwezo.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Mohamedi Punjan amesema wameguswa na matatizo mbalimbali ya watoto wenye ulemavu na kuamua kufika Tanzania kwa ajili ya kutoa msaada katika taasisi hiyo.
Taasisi ya Mohammed Punjan Foundation ya Kutoka nchi ya CANADA wamefika Tanzania kwa lengo la kusaidia watoto wenye ulemavu wa miguu na kuwapa Baiskeri za kutembelea pamoja na fimbo.Pia wametoa msaada kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa kuwapa msaada wa zaidi ya milioni 60.
UNAISHIWAJE PAWA KWA KUPANDA MLIMA LOLMALASIN ?
-
Wakati anamsifia mpenzi wake Msanii Mbosso aliimba “ _Kamusi namaliza
kurasa kukusifia”_ ,na akahitimisha kwa kusema anaishiwa pawa kwa kuwa
penzi la huyo...
Saa 15 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni