Wananchi wa mtaa virobo kata ya Chanika wamekuwa wakipata Huduma ya matibabu kwa wakati wa usiku kwa kutumia mwanga wa simu kutokana na kukosekana kwa umeme katika Zahanati ya Yangwe iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.
Kutokana na hali hiyo wadau wameombwa kusaidia kupatikana kwa umeme wa TANESCO kutokana na umeme uliopo wa jua kutokidhi ya mahitaji hospital hiyo.
Daktari wa zahanati ya Yongwe Ally Malika ameshukuru chama cha mapinduzi Wilaya ya Ilala kwa kuwapatia umeme wa sola.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala ndugu Kafuge Joel amewataka wananchi kuwa na subira sababu chama cha mapinduzi kinataka kuendelea kutekeleza Ilani kwa vitendo.Naye Mwenyekiti wa Mtaa akiongea amesema Serikali itahakikisha inaleta umeme katika Zahanati hiyo.
Licha ya kuwa Zahanati hiyo imesaidiwa umeme ila bado lina changamoto ya maji na upungufu wa wahudumu.
UNAISHIWAJE PAWA KWA KUPANDA MLIMA LOLMALASIN ?
-
Wakati anamsifia mpenzi wake Msanii Mbosso aliimba “ _Kamusi namaliza
kurasa kukusifia”_ ,na akahitimisha kwa kusema anaishiwa pawa kwa kuwa
penzi la huyo...
Saa 6 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni