RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA MABILIONEA, ALIKO DANGOTE NA BILL GATES

Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amepata nafasi ya kukutana na mabilionea wawili wakubwa duniani akiwa ziarani Davos nchini Uswisi.
Rais Jakaya Kikwete alikutana na tajiri namba moja Afrika, Alhaji Aliko Dangote kutoka nchini Nigeria na tajiri namba moja duniani, Bill Gates kutoka nchini Marekani.

Viongozi hao wamekutana nchini Uswisi katika Mkutano wa Dunia wa Uchumi (World Economic Forum) wenye lengo la kujadili mustakabali na mwenendo wa uchumi wa dunia.
Mbali na masuala ya uchumi, mkutano au kongamano hilo pia hujadili kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo kwa sasa yamekuwa ni tishio kubwa kwa viumbe mbalimbali.
Mkutano huu huudhuriwa na viongozi kutoka mataifa mbalimbali pamoja na asasi nyingine za kuraia zikiwa na lengo la kuweka nguvu pamoja na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List