Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, Jana Tarehe 02 Februari, 2017 amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.
Jenerali Venance S. Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Major Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.
Luteni Jenerali James M. Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Home / gloria media
/ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli ameteua Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania Mpya
- Blogger Comment
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Inaendeshwa na Blogger.
About Me
Wanaofuata
TANGAZO
My Blog List
-
-
SUPER D AMUANDAA SUNDAY KIWALE KWA USHINDI WA K,O JANUARY 31 TANGA ATAKAPOZIPIGA NA YOHANA MCHANJA - SUPER D AMUANDAA SUNDAY KIWALE KWA USHINDI WA K,O JANUARY 31 TANGA ATAKAPOZIPIGA NA YOHANA MCHANJA Na Mwandishi Wetu KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masum...Miaka 5 iliyopita
-
SUPER D AMUANDAA SUNDAY KIWALE KWA USHINDI WA K,O JANUARY 31 TANGA ATAKAPOZIPIGA NA YOHANA MCHANJA - Na Mwandishi Wetu KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa anamnowa bondia Sunday Kiwale 'Moro Best' kwa aj...Miaka 5 iliyopita
-
BONDIA MAKUBI ATAMBA KUMPIGA ABDALLAH MA MOROGORO OKTOBA 4 KATIKA UKUMBI WA 361 MWENGE - Na Mwandishi wetu Bondia Ibrahim Makubi yupo kambini kwa ajili ya mazoezi yake ya kumkabili bondia abdallah kingolwira wa ( morogoro ) katika pambano l...Miaka 5 iliyopita
-
JUMA CHOKI AJIANDAA NA MASHINDANO YA KING OF THE RING JULAI 28 - Bondia Ibrahimu Makubi kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa Mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Super D iliyopo shule ya Uhuru Kariakoo...Miaka 6 iliyopita
-
0 comments:
Chapisha Maoni