RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE ASISITIZA ELIMU KWA NCHI ZA AFRIKA KAMA UKOMBOZI WA MAENDELEO YA KIJAMII NA KIUCHUMI

Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kugharamia Fursa ya Elimu Duniani (UN Education Commission on Financing Global Education Opportunity) Ametumia fursa hiyo kama sehemu ya kuongelea ukombozi wa kimaendeleo ya kijamii kupitia elimu.

Mh Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete ametembelea nchi zaidi ya 14 afrika kuongelea fursa za elimu na jinsi ya kuboresha elimu ili kuleta maendeleo barani afrika.

Mh Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete richa ya kuwa na msukumo mkubwa katika masuala ya maendeleo afrika na ustawi wa jamii pamoja na kupigania dunia kuwa sehemu bora kwa maisha ya binadamu ameonekana kuamini Njia pekee ya kufanya watu wajifunze na kustawi ni kuboresha elimu.Karibuni katika mkutano wa wafanya biashara wakubwa duniani na wadau wa maendeleo kama Aliko Dangote Tajiri nambari moja afrika na Bill gates Tajari namba moja Duniani pia alipata fursa ya kuongelea ustawi wa nchi za afrika.

Pia Mh Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete kama Mjumbe maalum wakamisheni hiyo amekamilisha ziara yake ya kuhamasisha utekekezaji wa Ripoti ya Kamisheni hiyo ijulikanayo kama 'Kizazi Cha Elimu' (The Learning Generation).

Katika ziara hiyo iliyomfikisha katika nchi 15 imebeba ujumbe (report).Report hiyo inamapendekezo ya namna Dunia inavyoweza kukabili janga la Elimu kwa kuwekeza katika Mpango wa Kizazi cha Elimu(A Learning Generation). 

Mpango huo unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya Elimu katika nchi zinazoendelea ndani ya Kizazi Kimoja (miaka 30). Azma kuu ya Mpango huo ni kuwezesha ifikapo mwaka2040, watoto wote kote duniani wawe wanapata elimu iliyo sawa, na kwa kiwango cha ubora unaolingana dunia nzima.

Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa
Kamisheni ya Kimataifa ya Kugharamia
Fursa za Elimu Duniani Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Wakuu wa Nchi 12 kwa nchi za Uganda,Malawi, Msumbiji,Congo, Tunisia,Ghana,Chad, Gabon, Ivory Coast, Namibia,Afrika Kusini na Botswana.

 Aidha amekutana na Makamu wa Nigeria na Mawaziri Wakuu wa Ethiopia na Tanzania. Pamoja na viongozi wa nchi na Serikali.Rais Mstaafu amekutana na viongozi wa Taasisi za Kikanda 3 ambao ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Madhumuni ya ziara hizo yalikuwa ni
kufikisha ujumbe wa Kamisheni na Ripoti yake juu ya umuhimu wa nchi za uchumi wa kati na chini (low and middle income countries) kufanya mapinduzi makubwa ya elimu ili kukabiliana na janga kubwa la elimu linaloinyemelea dunia.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Kamisheni hiyo,
ubora wa elimu inayotolewa na nchi
zinazoendelea za uchumi wa kati na chini ni ile ambayo imetolewa na nchi
zilizoendelea miaka 70 iliyopita. Aidha,
nchi zinazoendelea ziko nyuma sana katika vigezo vitatu muhimu vya elimu vya fursa ya kujiunga na elimu (access to education), kumaliza elimu (completion) na ufaulu na kuelimika (learning outcomes). 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List