Rais Wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. John Pombe Magufuli leo Mei 29, 2017 amemwapisha Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo kuchukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye imeelezwa kuwa atapangiwa kazi nyingine.
Mara baada ya kuapisha, IGP Sirro amesema kuwa kati ya mambo ambayo atayashughulikia ni suala la uhalifu, ambapo ametoa onyo kali wa wote wanaotekeleza uhalifu akiwataka kuachana mara moja na tabia hiyo kwani si njema na wanahatarishia maisha yao.
Aidha, IGP Sirro amesema kuwa ili hayo yote yatekelezeke ni lazima uwepo ushirikiano mkubwa na nidhamu ili kuhakikisha Tanzania kwa ujumla inakuwa salama na wananchi waishi kwa amani.
0 comments:
Chapisha Maoni