Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameagiza usajili mpya wa wapiga kura wakati nchi hiyo inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Chini ya agizo jipya la serikali, raia wote Zimbabwe watakuwana miezi minne kujisajili upya katika daftari la usajili.
Zimbabwe itafanya uchaguzi mkuu mwaka ujao kwa kutumia dafatri hiyo mpya ya usajili wa wapiga kura , ikiwa ni mojawapo tu ya mageuzi ya uchaguzi yalioitishwa na upinzani kwa muda mrefu.
Agizo hilo la rais linasema usajili unapaswa kuanza September 14 hadi Januari mwaka ujao.
Mfumo huu mpya unaidhinishwa kwa kutumia vifaa vilivyonunuliwa hivi karibuni kutoka China.
Usajili utajumuisha kunakiliwa alama za vidole na ithibati ya ukaazi.
Dafatari hilo la usajili limekumbwa na mzozo katika uchaguzi wa siku za nyuma Zimbabwe.
Mnamo 2008 vyama vya upinzani vilisema waligundua makosa ikiwemo kusajiliwa kwa wapiga kura wengi waliokuwa wanasemekana kuishi katika eneo moja, na wengine katika maenoe yasioishi watu.
RAIS SAMIA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 61 YA MAPINDUZI YA
ZANZIBAR
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
ameshiriki maadhimisho ya kilele cha Miaka 61, ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar y...
Siku 2 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni