Viongozi wa dini nchini wametakiwa kusimamia masuala ya kiroho na kuachana kujiingiza kwenye Siasa ili kusimamia msingi ya Imani ili kudumisha Amani na utulivu nchini.
Hayo yamesemwa na mchungaji Stanley Joseph Ulomy wa Kanisa la Pentecost assemblies of God la Yombo vituka wakati wa Ibada maalumu ya kuombea Taifa amani.
Mchungaji Ulomy amewataka viongozi wa dini wasimame kwenye Karama walizopewa na sio kutoa maneno ya uchochezi wa kisiasa.
Mchungaji Ulomy amesema uwepo wa Rais John Magufuli ni Mpango wa mwenyezi Mungu hivyo inapaswa Viongozi wa dini waunge Mkono jitihada anazozifanya za maendeleo kwa ajili ya taifa.
0 comments:
Chapisha Maoni