Baada ya Kampeni za uchaguzi kumalizika rasmi nchini Tanzania.Mgombea Mahesh SHAH ameonekana kukubalika na kuwa kivutio cha wapiga kura wengi wa jimbo la Micheweni.
Mahesh Shah ambaye anasifika kuwa ni kijana mwenye maono na uwezo mkubwa wa kutambua changamoto na kushirikiana na watu katika kutatua changamoto hizo ameomba ridhaa ya chama cha mapinduzi kuwa mbunge wa jimbo la micheweni na kuwahasa wananchi wote kuwapigia kura wagombea wa chama cha mapinduzi kwa nafasi zote.
Kuelekea uchaguzi mkuu wananchi wameendelea kuguswa na kutoa maoni yao kwa wagombea waliomba nafasi za uongozi huku wakigusia utatuzi wa masuala mbalimbali yanayoikabili jamii.
Chama cha mapinduzi kimeendelea kukubalika Zanzibar na wananchi kuhaidi ushindi wa kishindo kwa Rais Mwinyi na wagombea wengine wa ccm.


0 comments:
Chapisha Maoni