Wakristo wote duniani wakiadhimisha siku ya kuzaliwa Mtoto Yesu Bethelemu wametakiwa kusherehekea kwa Upendo na Amani.
Baba Padre Joel Elia Kusupa wa Kanisa la Angrikana st Agnes lililopo Yombo Vituka wilaya Temeke Jijini Dar es salaam akiendesha ibada hiyo amesema Bwana Yesu Kristo amezaliwa katika Mazingira Magumu.Amezaliwa katika zizi la Ngombe sehemu wanyama kukuwepo vinyesi vya Wanyama amezaliwa katika Mazingira Magumu kwa maisha ya binadamu ya wasiwasi na Mashaka lakini Mungu yuko pamoja nao kumlinda na kumtetea,amesema binadamu wanapokuwa na magumu au matatizo mara nyingi Mungu hutokea na kutoa suluhu.
Kwa watu wenye matatizo uwapa nguvu,kuwafariji wanapo mtegemea Mungu. Umasikini si mpango wa Mungu hivyo unatakiwa kutegemea na kumwamini MUNGU.
Ujumbe wa Yesu Kristo ni Amani Upendo na Imani utowa katika hofu mahangaiko na kukuweka katika furaha. Maadhimisho hayo ya Sikukuu ya Krimas yalienda sambamba na kuwazadia zawadi akina mama Wajane na Watoto Yatima na Watoto wadogo walibatizwa katika Kanisa la Mtakatifu Sat Agnes Yombo Vituka jijini Dar es salaam .






0 comments:
Chapisha Maoni