Wazazi nchini wametakiwa kuwalea watoto katika maadili ya Mungu ili waweze kuwa na hekima,busara,imani na hofu ya Mungu.Vijana wanatakiwa kuwa nguvu kazi na sio magoigoi.
Hayo yamesemwa na Baba Askofu Jackson Sosthenes Jackson wa Mkoa Dar es salaam la Angrikana nchini wakati akiwapa kipaimara baada ya kuhitimu mafundisho. Kanisa la Sat Agenes Yombo vituka la Angrikana w lilaya ya Temeke jijini Dar es salaam Baba Askofu Jackson amesema watoto wanatakiwa walelewe kwa kupewa uhuru na kufundishwa Mipaka ya uhuru huo . Kuwandaa watoto kwa ajili Kesho kuliko kumuandaa kesho. Pamoja na kuwapenda kuwalinda kuwapa haki zao za msingi na kuwasikiliza. Itapunguza au kumaliza mmong'oyoko wa Maadili.Zaidi ya watoto 15 walipata Kipaimara.
Baba Padre Joel Elia Kusupa wa kanisa la st Agnes Yombo Vituka ametoa wito kwa watoto hao wakue kwa imani na kumtii Yesu Kristo.Kushiriki katika ibada na kuwa mabalozi kwa vijana wengine waondokane na makundi ya vijiweni.Wakimjua MUNGU watafanikiwa katika maisha yao.


0 comments:
Chapisha Maoni