MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amewapa rungu wana-CCM akiwataka kuacha kujifanya wanyonge dhidi ya vitendo vya fujo ambavyo hufanyiwa na Chadema nyakati za uchaguzi.
Rais Kikwete amesema hayo leo, wakati akiongoza kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini Dodoma.
"Uchaguzi wa Kalenga ndiyo huo upo mbele yetu, hadi sasa hakuna tatizo lililojitokeza kama Arumeru mambo yapo shwari kabisa, lakini tujue tu kwamba pale tunaenda kushindana na watu (Chadema) ambao wao silaha yao ya kwanza ni vujo.. ninaagiza sasa lazima wana CCM kukabiliana na fujo zao. Unyonge basi.", alisema Rais Kikwete na kuongfeza;
"CCM kuendelea kujifanya wanyonge kila mara sasa basi. Haiwezekazi watu wanafanya vujo hadi kuwatoboa watu macho ninyi nmanyongea tu, hili haliwezekani. Tazama pale Ingunga mtu wenu alimwagiwa tindikali hali leo ana ulemavu wa kudumu kisa uchaguzi tu, aah haiwezekani kabisa", alisema Rais Kikwete.
Mapema Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete alipongeza wana CCM na viongozi wao katika Kata zote zilizofanya uchaguzi mdogo wa Udiwani na hatimaye CCM kuibuka na ushindi wa Kata 23, Chadema ikiambulia tatu na NCCR Mageuzi kimoja.
Hata hivyo Rais Kikwete alisema, licha ya CCM kuzoa kata nyingi kwenye uchaguzi huo, viti vinne kwenda kwa upinzani bado ni doa hivyo lazima CCM ihakikishe inazikomboa kata hizo nyakati za chaguzi zijazo.
"Ni kweli tumezoa kata nyingi, lakini kwa kuwa lengo letu CCM kila wakati ni kushinda tu, hatua hiyo ya kuzikosa kata nne bado ni doa lazima kuzikomboa kata hizo chaguzi zijazo", alisema, Rais Kikwete.
Pia alipongeza CCM, kwa ushindi iliopata kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Kimbesamaki na kwamba CCM inaona fahari kulirejesha jimbo hilo mikononi mwake, kwa kuwa ilikuwa imelazimika kumfuza mwakilishi wake wa awali kwenye jimbo hilo kwa kuwa alikuwa msaliti aiyefaa kuendelea kuwemo ndani ya Chama.
0 comments:
Chapisha Maoni