Msaada toka wingereza toka Bi Gladness Sariah, na msaada toka DSM kwa Norah SilverBoutique |
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwakilisha msaada toka kwa familia ya mama Masawe wa DSM kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha NURU kilichopo Uyole Mbeya |
KITUO cha Mtandao wa kijamii cha Mbeya
yetu(www.mbeyayetu.blogspot.com)
kimepokea Misaada mbalimbali kutoka kwa wasamaria wema kwa ajili ya Kituo cha
kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole Jijini Mbeya na Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha
Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa
mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya
Wazazi ya META jijini Mbeya.
Msaada wa kwanza ulipokelewa hivi
karibuni wenye thamani ya shilingi Laki Moja kutoka Familia ya Masawe wa Dar Es
Salaam kwa ajili ya kituo cha Nuru ambapo Mbeya yetu iliuwasilisha kama ulivyo.
Aidha katika kuonesha wengi wameguswa na
tukio la Mwanamke huyo kujifungua watoto wanne ambao wanaendelea vizuri pia Msamaria mwema mwingine aliyejulikana kwa jina la Dada Norah SilverBoutique toka DSM ambaye
ametoa Maziwa Lactogen Dazan Mbili yaani makopo 24 pamoja na nguo ambavyo
vimewasili salama katika ofisi ya Mbeya Yetu.
Shukrani kwa Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya
huko Uingereza na ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha kufika kwa mizigo hii Mbeya.
Kutokana na kupokelewa kwa mizigo hiyo
ambapo kituo cha Nuru kilikabidhiwa Katoni Mbili za Sukari, Sabuni na Biskuti
pia Tunatarajia kuanza safari ya
kwenda huko Chiwanda Wilaya ya Momba Kilomita zaidi ya 260 kwenda na kurudi kesho majira ya saa Moja asubuhi.
Hivyo ni wito wetu kwenu kuendelea
kutuombea na kutuunga mkono katika safari hiyo ili tuweze kuifikisha salama
mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia maendeleo ya Watoto hao ambapo
watakuwa wameshatimiza mwezi mmoja na siku 24.
Tunawashukuru sana tena sana mungu
awabariki.
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada
tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com
nasi tutafikisha ubani wako.
Serengeti Freight wametoa ofa ya
kusafirisha bure misaada ya aina
Na Mbeya yetu
0 comments:
Chapisha Maoni