Dihile (chini) |
Akizungumza na MICHARAZO, Dihile alisema bado yupo sana dimbani katika kuendelea kucheza soka akiamini uwezo na umri unamruhusu kufanya hivyo kwa muda mrefu.
Dihile, alisema kwa nafasi ya kipa kadiri umri unavyosonga mbele ndivyo uimara wa makipa unavyoimarika na kwamba hadhani kama atatundika 'glovu' zake mapema katika misimu ya karibuni.
"Sijafikiria kustaafu kwa sasa, bado najiona nina uwezo na umri wa kuendelea kucheza kwa muda mrefu, japo kustaafu kunategemea mambo mengi ukiacha suala la umri," alisema.
Alisema kupata majeraha makubwa ni sababu inayowaondoa wachezaji uwanjani na kwa bahati nzuri yeye hajawahi kupatwa na kitu hicho hivyo haoni sababu ya kutundika glovu zake kwa sasa, labda kama ataamua mwenyewe kwa masuala mengine ikiwamo kutaka kuzisimamia miradi yake ya biashara anayoiendesha kwa sasa.
"Ya Mungu mengi, naweza kufanya maamuzi hayo labda kutaka kusimamia biashara zangu, lakini kwa sasa zinaendelea vyema ndiyo maana sina mpango wa kustaafu kwani najiona bado sana kisoka," alisema Dihile aliyewahi kuichezea Pan Africans ya jijini Dar.
Nahodha wa JKT Ruvu, Hussein Bunu alinukuliwa na MICHARAZO katika mahojiano yake maalumu wiki iliyopita akidai huu ni msimu wake wa mwisho kucheza kwa vile atatundika 'daluga' zake na kujikita kwenye ukocha aliouanza kwa sasa.
0 comments:
Chapisha Maoni