Donovan "Razor" Ruddock
Vs Lennox Claudius Lewis
HILI lilikuwa ni moja ya mapambano yaliyowavuta mashabiki wengi wa ngumi duniani, na hasa kutokana na umahiri wa mabondia wote wawili.
Ilikuwa ni katika mji wa Halloween, Oktoba 31, 1992 katika ukumbi wa Earls Court jijini London, Uingereza ambako mabondia hao walikutana.
Kwa upande wa Lennox Lewis, ilikuwa ni kipimo cha uhakika kwani hilo lilikuwa pambano lake la kwanza kukutana na bondia wa 'ukweli' Donovan "Razor" Ruddock aliyeogopwa kwa ngumi nzito na zenye nguvu.
Ruddock alikuwa ni mpiganaji wa kiwango cha juu duniani, wenyewe wanasema 'world class fighter'. Awali alikuwa amemuhenyesha sana Mike Tyson katika mapambano yao yote mawili, lakini pia Ruddock alikuwa amemchana chana bingwa wa zamani Michael Dokes.
Lakini umuhimu mwingine wa pambano hilo lilikuwa ni la kumtafuta atakayewania ubingwa dunia wa WBC kwa kupambana na Riddick Bowe aliyekuwa mtetezi wa mkanda huo.
Je, Lewis atakuwa bingwa wa dunia kutoka Uingereza baada ya miaka 100 tangu afanye hivyo Henry Cooper na Bob Fitzsimmons ambaye alikuwa wa mwisho kubeba ubingwa wa dunia akiwa Muingereza? Ndilo swali lililokuwa likiulizwa na mashabiki wengi wa ngumi hasa wa Uingereza.
Hakuna aliyedhani kuwa pambano hilo lingekuwa jepesi, Lewis alikuwa ni bondia anayeheshimika kwa kuwa bingwa wa medali ya dhahabu (Olympic Gold Medalist) lakini pia hadi katika pambano hilo alikuwa hajapoteza hata moja.
Alishawadunda mabondia kama Tyrell Biggs, Mike Weaver na Gary Mason, lakini hakuwahi kupata pambano dhidi ya bondia anayesifika na kuogopwa kwa nguvu na uzito wa ngumi kama Razor, kwa hakika huu ulikuwa mtihani mkubwa kwa Lewis.
*Pambano
Ilishitusha, wengi hawakuamini lakini ndivyo ilivyokuwa, pambano hilo likawa jepesi ajabu kwa Lewis ! Hakuna aliyeweza kutabiri kama Lewis angeshinda pambano hilo kwa ulaini kiasi kile lakini kocha wake wa zamani, Pepé Correa alidai kwamba alitabiri ushindi wa mapema kwa Lewis.
1. Raundi ya kwanza:
Mabondia wote wanaitwa kusalimiana katikati ya ulingo, wanakutana na kutizamana uso kwa uso, Ruddock anamwangalia Lewis kwa macho ya ukali na vitisho, lakini Lewis anakuwa mpole kama pande la barafu.
Nakukumbusha tu kuwa Lewis kabla ya kuchukua uraia wa Uingereza alikuwa na uraia wa Canada. Ruddock naye ni mzaliwa wa Canada, wote walikuwa kwenye timu ya ngumi ya taifa ya ridhaa na walikuwa wanajuana vizuri. Lewis ana uraia wa Uingereza na Canada.
Baada ya kusalimiana katikati ya ulingo, kila mmoja anarudi kwenye kona yake huru (neutral corner) kisha kengele inalia kuashiria raundi ya kwanza. Ruddock anakuwa wa kwanza kutoka kwenye kona yake na kumfuata kwa nguvu Lewis.
Mabondia wote wanashambuliana kwa tahadhari, wanaonekana wakiwa na nguvu za miili na wakiwa katika hali nzuri, hiyo inafanya wachambuzi wa ngumi kuamini kwamba pambano hilo litakwenda raundi nyingi.
Lakini wakati raundi ya kwanza inaelekea ukingoni, linatokea tukio la kustajaabisha! Ruddock, anafanya kosa la mwaka, anapiga ngumi ya kudonoa ya kushoto (left jab) katika chembe ya kifua cha Lewis, na wakati mkono wake ukiwa umenyooka, anakuwa ameacha uwazi kwenye taya lake la kulia.
Lewis anaioa nafasi hiyo, anaona namna taya la Ruddock lilivyobaki 'uchi' (wazi), hana muda wa kupoteza, anakaza msuli wa mkono wake wa kulia na kushusha fataki kali linalokamata shabaha sawia!
Ngumi ile ya kulia (right ), inatua kwenye taya la Ruddock (vitendo hivyo vyote vinatokea haraka sana katika muda wa sekunde mbili u )
Ngumi ile inamwingia Ruddock vizuri miguu yake inakosa nguvu na anabinuka na kuanguka chini kama furushi la dagaa wa Mwanza! Kwanza umati unashangaa kisha unashangilia kwa mshangao! Wanashangaa nguvu ile ya ngumi Lewis alikoipata!
Lakini wakati Ruddock anajizoa pale chini, kengele ya kuashiria kumalizika kwa raundi ya kwanza inalia na hivyo mwanamume anaokolewa na kengele katika raundi ya kwanza, anakwenda kwenye kona yake na ulevi wa sumbwi lile.
Kocha wa Ruddock, Floyd Patterson, anamwambia bondia wake kutulia na kumjenga kisaikolojia kwa ajili ya raundi ya pili, lakini kwa hakika ngumi ile aliyodundwa Ruddock imemuumiza vibaya hakuwa ngumi ya mzaha, lilikuwa ni kombora.
2. Raundi ya Pili:
Raundi ya pili inapoanza, Lewis anakuwa na tahadhari zaidi, pengine anakumbuka umahiri wa Ruddock ambaye katika mpambano yake alishwahi kupigwa na kudondoka chini lakini akaja kushinda.
Razor anaendelea na mashambulizi katika raundi hii, anaachia 'right' kali ya kulia na inatua kichwani kwa Lennox ambaye anajikaza na kujibu shambulizi hilo.
Lennox anajibu kwa mchanganyiko wa ngumi (combination), kumbuka mkono wa kushoto wa Lewis ni kama risasi, unafyatuka kwa haraka na Rudock anashindwa kuziona 'jabs' kadhaa zinazodondokea usoni mwake na kisha ngumi nyingine ya kulia inafuatia na kutua kwenye kichwa chake, Ruddock anakwenda chini kama mlevi wa kangara kwa mara ya pili katika pambano hilo.
Ruddock anahesabiwa na kunyanyuka lakini akiyumba kwa ulevi na mwamuzi anaporuhusu pambano liendelee,
Lewis anachomoka spidi lakini kwa tahadhari ya kwenda kummaliza Ruddock.
0 comments:
Chapisha Maoni