LG yazindua jokofu lenye kutunza baridi kwa muda mrefu.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Hotpoint Tanzania BW.
Mayur Parikh wa pili kushoto na meneja masoko wa kanda wa kampuni hiyo
BW, Shakti Vellu wakizindua Jokovu lenye kutunza baridi la kampuni ya LG
picha na www.burudan.blogspot.com
Feb 14, 2014: Kampuni ya vifaa vya Umeme ya LG leo imezindua jokofu la kisasa
zaidi yenye uwezo wa kutunza ubaridi kwa muda wa masaa saba upande wa jokofu ya
kawaida na masaa kumi kwa upande wa friza hata pindi umeme unapokuwa umekatika.
Bidhaa hii mpya imezinduliwa mahususi kutokana na tatizo lililo
kithiri la katizo la umeme ambalo hukumba maeneo mengi ya nchi na kusababisha
vifaa vya umeme kukosa matumizi kwa muda mrefu.
Aidha tatizo hili la kukatika kwa umeme mara kwa mara kumepelekea
makapuni kama LG kutanua wigo wao katika kutafuta suluhu na hivyo kubuni teknolojia zenye usasa uliopindukia katika
ubunifu wa vifaa vitavyo himili nyakati umeme unapokosekana. Ni katika ubunifu
huo ndipo LG ikatengeneza jokofu hili jipya lisilogandisha barafu kwenye
“friza” linaloweza kutunza ubaridi katika sehemu ya ‘friji” kwa zaidi ya masaa
saba hasa pale umeme unapokatika kwa kipindi kirefu.
Akiongea siku ya uzinduzi Appliances
Product Manager LG East Africa, Oktae Kim alisema uzinduzi huu umelenga
katika ubunifu mkubwa unaohusiana na mahitaji ya mteja na jinsi ya kuyatatua.
Hivyo basi tunajitahidi kubuni bidhaa ambazo zina kidhi mahitaji ya wateja
wetu.
Teknolojia iliyotumika inahusianisha valve kwenye jokofu ambayo
hufunguka pale ambapo kunapokosekana na umeme. Valve hii inasambaza ubaridi
kwenye vifaa vingine vilivyoundwa maalumu kutunda ubaridi na pindi umeme
ukatikapo vipaa hivi huanza kutoa ubaridi kwa muda wa saa saba.
Bwana Kim amesema: “Evercool
inapooza mara tatu zaidi kwa
kutumia evaporator tatu. Evaporator kuu inatumia umeme na mbili zinafanya kazi
bila kutumia umeme. Kwa hiyo sasa unaweza kufaidi vinywaji baridi na kuepuka
kuharibika kwa chakula chako kwenye jokofu mara umeme unapokatika”.
LG ina visahani vya kugandishia barafu ambavyo vina uwezo wa
kugandisha barafu kwa haraka ya zaid ya asilimia 20. Imetengenezwa kwa umahiri
na maeneo ya kutosha kwa ndani na hivyo kukuwezesha kupata sehemu ya kutosha
ndani wakati wa kuweka vitu. Sasa unaweza kutunza mboga na matunda vizuri bila
kuogopa vitu kuharibika kutokana na mrudikano wa vitu nahivyo kusababisha
unyevunyevu unaopelekea kuharibu vyakula. Na wakati wa kipindi cha joto kali,
jokofu hili la milango miwili litakushangaza kwa kutunza chakula kwa hali ya
juu.
Pia mwanga wa LED unang’aa
zaidi, unadumu kwa muda mrefu na unatumia umeme mdogo. Na mtu atakayenunua
jokofu hili hahitaji kutafuta ‘Stabilizer” kwani jokofu hili linaweza kufanya
kazi vizuri hata wakati umeme unapokuwa mdogo.
Bw. Kim aliongezea kwakusema :compressor za LG ni Imara na
tunakupa guarantee ya mwaka mzima” Pia aliongeza kuwa wanajitahidi kuhakikisha
wanaendelea kuzalisha bidhaa za kisasa na zinazoendana na mahitaji halisi ya
watu.
0 comments:
Chapisha Maoni