picha kwa hisani ya mitandao ya kijamii.
Mbunge
wa jimbo la Iringa mjini Mh.PETER MSIGWA kwa mara nyingine amefikishwa
leo katika mahakama kuu ya mkoa , kufuatia tuhuma inayomkabili ya
kufanya vurugu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata
ya nduli manispaa ya iringa.
Tukio
hilo limetoke tarehe 6 ya mwezi wa pili ambapo SALUM KEITA mjumbe wa
kampeni hizo kupitia chama cha mapinduzi alidai kufanyiwa vurugu na
mbunge wa jimbo la iringa mjini kwa kumpiga.
Kesi
hiyo imesomwa leo katika mahakama ya wilaya ya Iringa mbele ya
jaji ALOYCE MASUA na kesi hiyo imeahirishwa na kutajwa kusikilizwa
tarehe 9 ya mwezi wa 4 mwaka huu.
0 comments:
Chapisha Maoni